Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akizungumza na Daktari wa timu ya Taifa Stars Emily Urasa wakati wa kuwafanyia
uchunguzi wa kina wa magonjwa ya moyo wachezaji wa timu hiyo leo Jijini Dar es
Salaam. Wachezaji hao walifanyiwa vipimo
vya kuangalia jinsi moyo
unavyofanya kazi (Echocardiograph) na
mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography –ECG).
Daktari
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Siza Ngomero akimpima kipimo Error!
Not a valid embedded object.cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiogram)
mchezaji wa timu ya Taifa Stars Feisal Salum wakati wa uchunguzi wa kina wa
magonjwa ya moyo kwa wachezaji wa timu hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Fundi
Sanifu wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abuu
Dalidali akimpima kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electricalcardiography –ECG)
mchezaji wa timu ya Taifa Stars Yahaya Zaid wakati wa kuwafanyia uchunguzi wa
kina wa magonjwa ya moyo wachezaji wa timu hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao wamefanyiwa uchunguzi wa kina wa magonjwa ya moyo kabla ya kwenda
nchini Misri kushiriki mashindano ya AFCON yatakayoanza tarehe 21/06/2019. (PICHA NA: GENOFEVA MATEMU – JKCI)
Wachezaji 38 wa timu ya Taifa Stars wamefanyiwa
uchuguzi wa kina wa magonjwa ya moyo kama Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF)
linavyoelekeza kabla ya kuanza kwa mashindano ya kombe la Mataifa ya Africa (AFCON)
ni lazima wachezaji wanaoshiriki
mashindano hayo wapimwe afya zao.
Vipimo walivyofanyiwa wachezaji hao ni
vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi
(Echocardiograph) na mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi
(Electrocardiography –ECG). Upimaji huu umefanywa na madaktari bingwa wa
magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI).
Taasisi yetu ni Hospitali
iliyothibitishwa na CAF kuwa inakidhi
vigezo vyote vya upimaji wa magonjwa ya moyo. Uthibitisho huu ulitolewa kabla
ya kuanza kwa mashindano ya AFCON kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
yaliyofanyika mapema mwaka huu hapa nchini .JKCI ilikaguliwa na kuthibitishwa
na wakaguzi kutoka CAF.
Matokeo ya vipimo hivyo yatasaidia
kufahamu afya za wachezaji na utimamu
wao wa kimwili kabla ya kwenda kushiriki
katika mashindano ya AFCON yanayotarajia
kuanza tarehe 21/06/2019 huko nchini
Misri.Tunatoa
wito kwa vilabu vya mpira hapa
nchini kuwaleta wachezaji wao kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa
magonjwa ya
moyo hii itawasaidia wachezaji hao kufahamu kama wanamatatizo au la na
kuepukana na vifo vya ghafla vinavyoweza kuwapata wakiwa uwanjani. Kwa
upande wa wananchi kabla ya kujiunga na vilabu vya mazoezi ni
muhimu wakapima afya zao yakiwemo
magonjwa ya moyo..

No comments :
Post a Comment