Monday, June 10, 2019

TAKUKURU Yatimiza Agizo la Rais Magufuli....Watumishi Hawa Kuburuzwa Mahakamani


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo Jumatatu Juni 10, 2019  imewataja askari polisi wawili na mtumishi mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliohusika na ukamataji pamoja na uzuiaji wa mizigo wa mfanyabiashara Ramadhani Ntunzwe.

Takukuru imewataja watumishi hao ni Charity Ngalawa ambaye ni mwajiriwa wa TRA makao makuu, askari Polisi PC Simon Sungu pamoja na askari polisi PC Ramadhani  Uweza wote wakitokea kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Athuman Diwani imesema watumishi hao wanatuhumiwa kwa kosa la kuomba rushwa ya Sh2 milioni kutoka kwa mfanyabiashara huyo kinyume cha kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya 2007.

No comments :

Post a Comment