Monday, June 10, 2019

. Mkurugenzi Shule ya Lucky Vincent na Makamu Mkuu wa shule hiyo Wahukumiwa na Mahakama kufuatia kukutwa na hatia baada ya ajali iliyoua wanafunzi 32.


Mkurugenzi wa Shule ya Lucky Vincent, Innocent Mushi amehukumiwa kifungo cha miaka 4 au faini ya Sh. Mil. 1.5, huku Makamu Mkuu wa shule, Longino Vicent akihukumiwa mwaka 1 au faini ya Sh. laki 5, kufuatia kukutwa na hatia ya makosa 5 baada ya ajali iliyoua wanafunzi 32.

Hukumu ya kesi hiyo imesomwa leo Jumatatu Juni 10, 2019 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama, Niku Mwakatobe.


Ajali hiyo, ilitokea Mei 6, 2017, katika eneo la Rhotia wakati, wanafunzi wa shule hiyo, wakitoka Arusha majira ya saa 12 asubuhi kwenda wilayani Karatu, katika mitihani ya ujirani mwema katika Shule ya Tumaini Academy.

Makosa hayo matano ambayo Hakimu Mwakatobe amewakuta na makosa hayo matano ni; kuvunja sheria za usalama barabarani ikiwemo kuendesha gari za abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji, gari lililosababisha ajali kutokuwa na bima, kushindwa kuingia mkataba baina ya dereva na mwajiri na kosa la kuzidisha abiria 13 katika gari lililopata ajali ambalo linamkabili mwalimu mkuu msaidizi.


Hata hivyo, Washtakiwa hao walifanikiwa kulipa faini hiyo na kuachiwa huru.

No comments :

Post a Comment