Spika
wa Bunge Job Ndugai anatarajiwa kuwaongoza Wabunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kushuhudia mashindano ya Mataifa ya Afrika
(AFCON) Nchini Misri.
Mashindano
hayo yanayotarajiwa kuanza June 21 mwaka huu nchini Misri ambapo
Tanzania imepangwa Kundi C pamoja na Nchi za Kenya, Algeria na Senegal.
Akizungumza
leo Juni 10, bungeni mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali
na majibu, Spika Ndugai amesema ataenda kushuhudia fainali hizo.
“Na
wale wa awamu ya kwanza kama siku zile nne ni chache na mimi nitalipia
nitaenda na wale wa awamu ya kwanza hivyo tunaweza kuwa
pamoja,”amesema.
Akizungumzia utaratibu wa safari na gharama zake, Spika Ndugai amesema kutakuwa na awamu mbili za safari za kwenda Nchini Misri.
“Awamu
ya kwanza ambayo itakuwa ya siku nne gharama zake ni Dola za Marekani
720 ikijumuisha tiketi za kwenda na kurudi, usafiri wa kwenda uwanjani
na kurudi hotelini na malazi.
“Mwenyekiti
wa Bunge Sc Club, William Ngeleja, anaawatangazia na kuwaombeni kwa
ambao tunapenda kushuhudia fainali za AFCON nchini Misri mwaka huu
tuendelee kujiandikisha kupitia kwake, Ester Matiko, John Kadutu,Venance
Mwamoto, Sixtus Mapunda na Cosato Chumi wale ambao tungependa kwenda.
“utaratibu
mzima wa safari umeishatolewa kupitia mitandao yetu ya bunge gharama za
safari unachagua mwenyewe kama unataka kwenda awamu mbili ama
moja,”amesema Ndugai.
Amesema awamu ya pili ambayo itakuwa ya siku sita gharama zake ni dola za Marekani 770 kwa kichwa.
“Awamu
ya pili ni ya siku sita hii gharama zake ni dola 770 tu kwa hiyo
ukitaka kukaa siku zote ni sawa tu, ‘Atleast’ awamu mojawapo waheshimiwa
Wabunge tunaweza tukashiriki, ”amesema.
Aidha Spika amewaomba Wabunge kwenda kuiunga mkono Taifa Stars ili wachezaji wajione wanadeni kwa taifa.
“Tunaomba
sana waheshimiwa Wabunge tuunge mkono sana timu yetu ni miaka mingi
sana hatujafika AFCON kwahiyo wachezaji wakiwa wanacheza wanaona wabunge
wamekuja kuwaunga mkono naamini itawapa nguvu kubwa zaidi,”amesema.
No comments :
Post a Comment