Mwanafunzi wa chuo kikuu anauguza
majeraha baada ya maafisa wa polisi kumpiga risasi wakati akijaribu
kuruka ukuta kuingia Ikulu usiku wa Jumatatu, Juni 10,2019.
Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Kilimo
na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) kwa jina Brian Kibet Bera,
alikuwa amebeba kisu wakati wa tukio hilo.
Brian Kibet, mwanafunzi huyo wa Chuo
Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) alikuwa amebeba
kisu wakati wa tukio hilo.
Baadaye Kibet mwenye umri wa miaka 25,
ambaye ni mwanafunzi wa somo la uhandisi wa mitambo, alipelekwa katika
Hospitali Kuu ya Kenyatta huku uchunguzi ukianzishwa kubaini
alichokusudia.
Polisi wanasema Kibet alipanda kwenye
lango na alichomoa kisu baada ya kuamriwa na polisi kujisalimisha na
alipokataa, walinzi walimfyatulia risasi begani.
Baadaye Kibet mwenye umri wa miaka 25,
ambaye ni mwanafunzi wa somo la uhandisi wa mitambo, alipelekwa katika
Hospitali Kuu ya Kenyatta huku uchunguzi ukianzishwa kubaini
alichokusudia.
Kulingana na ripoti ya polisi, mshukiwa huyo atazuiliwa katika kituo cha Polisi cha Kileleshwa baada ya kutoka hospitalini.
Mwaka wa 2015, mwanafunzi mwingine
Matthew Kinuthia Maina, aliingia Ikulu na kushtakiwa kortini kwa kosa la
kuingia katika eneo lenye usalama mkali bila idhini.
Maina alijitetea kwa kusema kuwa alikuwa
na msukumo mkubwa wa kutaka kukutana Rais Uhuru Kenyatta kujadili
masuala kuhusu masomo.
"Kweli niliruka kuingia State House
kwa sababu nilijua nitampata rais hapo. Nataka anisaidie na pesa niweze
kurekodi muziki wangu ili niweze kupata karo ya shule" Maina aliambia korti wakati akijitetea.
No comments :
Post a Comment