Mkurugenzi wa MISA Tanzania Gasirigwa Sengiyumva akichangia mada katika warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari.
Geline Fuko (kushoto) akiwasilisha mada wakati wa siku ya pili ya warsha hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Network of Legal Aid Provider Christina
Kamili (kulia) akiwasilisha mada wakati wa siku ya pili ya warsha hiyo.
Na Mwandishi Wetu
Katika kuendeleza hamasa na kutetea uhuru wa kujieleza katika jamii,
MISA Tanzania na shirika la utetezi wa sheria na haki za kijamii la ICNL
zimewakutanisha wadau mbali mbali katika warsha ya utetezi wa sheria za
vyombo vya habari.
Warsha hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya habari,asasi
za utetezi wa haki za binadamu, wanasheria pamoja na wahadhiri wa vyuo
vikuu.
Warsha hiyo ya siku tatu iliyofanyika mjini Bagamoyo ambayo ni
muendelezo wa warsha iliyofanyika mwezi Machi mwaka huu ililenga
kuwakutanisha wadau hao kwa lengo la kujadili zaidi namna sheria za
vyombo vya habari zinavyo athiri mazingira ya kazi za kiuandishi pamoja
na uhuru wa kujieleza.
Bw.Aloys Habimana kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za
kijamii la ICNL akiendesha warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya
habari iliyoandaliwa na kuendeshwa na MISA kwa kushirikiana na shirika
la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL.
Kadhalika akielezea umuhimu wa uwepo wa sheria rafiki katika kufanya
mazingira yawe salama kwa tasnia ya habari,Bw.Aloys Habimana kutoka
shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL lenye makao
makuu yake nchini Marekani amesema changamoto ya sheria zisizo rafiki
kwa taaluma ya habari na uhuru wa kujieleza ni changamoto sehemu nyingi
duniani Afrika ikiwa na mifano halisi.
"Pamoja na mazingira haya nawasihi msivunjike moyo wala kukata tamaa,
masuala ya kisheria hayabadiliki kwa siku moja yanahitaji kupitia hatua
kadhaa na kila jambo linaweza kupatiwa ufumbuzi hasa wadau wote
watakaposhirikiana na kujenga hoja zenye ushawishi na tija kwa pande
zote", alisisitiza Bw.Aloys.
Bi.Lily Liu kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la
ICNL akijadili jambo pamoja na wadau walioshiriki warsha hiyo.
Sambamba na hilo Bi.Lily Liu mjumbe kutoka ICNL aliahidi kuwa shirika
lao litaendelea kushirikiana na wadau husika katika nyanja zote ili
kufanikisha na kutimiza adhma ya kuwa na jamii isiyo na sheria kandamizi
zinazoathiri dhana nzima ya uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari.
Warsha hiyo iliyojikita zaidi katika mfumo wa washiriki kubadilishana
mawazo na uzoefu wao wa mazingira ya kazi pamoja na namna hali
inavyobadilika na kubanwa kwa uwepo wa sheria zisizojitosheleza.
Washiriki warsha hiyo wakijadili baadhi ya sheria na kanuni katika makundi.
Mkurugenzi wa Highlands Fm Radio ya Mbeya Bi. Jacqueline Lawrence akiwasilisha mada kwa niaba ya washiriki wenzake
Washiriki wa warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari
iliyoandaliwa na kuendeshwa na MISA kwa kushirikiana na shirika la
kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kufungwa kwa warsha hiyo.
Pages
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment