SPIKA
wa bunge Mhe. Job Ndugai ameliambia bunge jijini Dodoma jioni hii ya Juni 28, 2019 kuwa ubunge wa Mbunge
wa jimbo la Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu (pichani) umetenguliwa.
Spika
Ndugai amesema hatua hiyo ni baada ya Mhe. Tundu Lissu kuvunja Katiba ya
nchi kwa kutowasilisha taarifa za... mali zake kwenye Tume ya Maadili ya
Viungozi wa Umma, lakini pia kutohudhuria mikutano ya bunge bila ya
kutoa taarifa.
Ni
kweli kila mmoja wetu anajua nini kilichomtokea Mhe. Tundu Lissu,
ambalo alipelekwa Nairobi kwa matibabu na baadaye kuhamisjhiwa Ulaya
kuendelea na matibabu. Hata hivyo kwa muda mrefu Mheshimiwa Tundu Lissu
amekuwa akionekana kwenye mijadala mbalimbali akihutubia mikutano na
makongamano mablimbali huko Ulaya.
“Katika mazingira yote mawili
ubunge wake unakoma na ataacha kiti chake cha ubunge jimbo la Singida Mashariki, na tayari Ofisi ya Spika
imekwishatoa taarifa kwenye Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kuhusu suala hilo.
No comments :
Post a Comment