Kaimu
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), ambaye pia ni Meneja
Masoko na Mauzo, Bw, Januarius Maganga(wapili kulia), akizungumza jambo
na Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi
wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, (wakwanza kushoto), wakati
alipotembelea kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Juni 11, ikiwa ni ziara
ya kujenga mahusiano lakini pia kueleza shughuli za Mfuko huo ambao
umeanza kutekeelza majukumu yake Agosti 2018 baada ya serikali
kuiunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, LAPF, PPF na
GEPF.
Meneja
Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF), Bi. Eunice Chiume, (wakwanza kushoto), akiwa na Afisa Uhusiano
Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi (wapili kushoto), wakiwa
kwenye mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya magazeti ya serikali (TSN),
chini ya Kaimu Mhariri Mtendaji, Bw. Januarius Maganga (wakwanza kulia),
ikiwa ni muendelezo wa ziara ya meneja huyo kiongzi kutembeela vyombo
vya habari kwa nia ya kujenga mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo
mpya.
Meneja
Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akifafanua masuala mbalimbali kuhusu
shughuli na majukumu ya Mfuko huo.
Meneja
Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akifafanua masuala mbalimbali kuhusu
shughuli na majukumu ya Mfuko huo.
Kaimu
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), ambaye pia ni Meneja
Masoko na Mauzo, Bw, Januarius Maganga, akizungumza mbele ya mgeni wake
Bi. Eunice Chiume wakati wa mazungumzo yao
Picha ya pamoja na uongozi wa TSN.
Meneja
Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Azam Media, Bw. Tido Mhando, wakati alipotem,belea vyombo vya habari vya
kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Juni 11, 2019.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Bw. Tido Mhando, (kushoto), akisalimiana
na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi wakati wa ziara
ya kutembelea vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni hiyo jijini
Dar es Salaam.
Meneja
Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF), Bi. Eunice Chiume(wapili kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi
wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, wakiwa katika mazungumzo na Afisa
Mtednaji Mkuu wa Azam Media, Bw. Tido Mhando (wapili kushoto) na Meneja
Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. John Mbele wakati wa ziara ya
meneja huyo kwenye vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni hiyo vya
Azam TV na Uhai FM.
Meneja
Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF), Bi. Eunice Chiume(wapili kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi
wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, (watatu kushoto), wakiwa katika picha
ya pamoja na watangazaji mashuhuri wa luninga ya Azam TV, Charles
Hillary na Ivona Kamuntu.
Picha ya pamoja
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications, Bw. Francis Nanai
(kulia), akisalimiana na Meneja Kiongozi Uhusiano wa PSSSF, Bi. Eunice
Chiume, (wapili kushoto) huku Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw.
Bakari Machumu akishuhudia wakati wa ziara ya meneja huyo ikiwa ni
muendelezo wa kutembelea vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Juni 11,
2019.
Mhariri
Mtendaji wa gazei la Mwananchi, Bw. Frank Sanga (kulia), akiongozana na
Bi. Eunice Chiume, wakati alipotembelea chumba cha habari cha kampuni
ya Mwananchi Communications Tabata jijini Dar es Salaam Juni 11, 2019.
Meneja
Kiongozi Uhusiano wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume, (wapili kushoto) na Bw.
Abdul Njaidi (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na
watangazaji wa kipindi cha XXL, cha Clouds FM, kutoka kushoto, B12,
Kennedy the Remedy, na DJ
Picha ya pamoja na uongozi wa Clouds Media
JUMLA
ya wastaafu elfu 10,500 bado hawajafika kwenye ofisi za Mfuko wa...
Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), ili kuhakiki taarifa zao
hadi sasa, Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko huo Bi. Eunice Chiume
ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati akitembelea vyombo vya habari
jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2019.
Vyombo
vya habari alivyotembelea leo Juni 11, 2019 kwa lengo la kujenga
mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo ambao ni Mpya ni pamoja na
magazeti ya serikali yanayomilikiwa na kampuni ya Tanzania Standard News
Papers (TSN), Azam Media, wamiliki wa Azam TV na Uhai FM, Mwananchi
Communications Limited, wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, Citizen
na Mwanaspoti na Clouds Media Group, wamiliki wa Clouds TV na Clouds FM.
Alisema,
zoezi la kuhakiki taarifa za wastaafu huwa linafanyika kila mwaka na
huu ni utaratibu wa taasisi za hifadhi ya jamii na kwa upande wa PSSSF
zoezi lilianza Desemba mwaka jana (2018).
”Tangu
Mfuko huu uanze shughuli zake Agosti 1, 2018 PSSSF ilifungua ofisi nchi
nzima Bara na Visiwani na hivyo tunatoa wito kwa wastaafu wote ambao
bado hawajahakiki taarifa zao kufanya hivyo kupitia ofisi zetu
zilizoenea nchi nzima na wala hawalazimiki kuja makao makuu Dodoma
kupatiwa huduma hiyo. “Alifafanua Bi. Eunice Chiume.
Zoezi
la kuhakiki taarifa hufanyika kila mwaka kwa upande wetu tulianza zoezi
hili Desemba mwaka jana (2018) na liliendelea hadi Machi 2019 na
tumeanza tena na zoezi hilo nab ado linaendelea.
“kuhakiki
taarifa ni muhimu kwani kunasaidia kujiridhisha na taarifa za wastaafu
wetu kwa sababu huwa kunakuwa na mabadiliko mbalimbali ikiwa ni pamoaja
na kujua kama bado wapo, au taarifa zao za kibenki zimebadilika au la
nah ii inasaidia kufanya malipo sahihi na kwa mtu sahihi.” Alibainisha.
Meneja
huyo Kiongozi alitoa wito kwa wastaafu na jamii kwa ujumla kuwa PSSSF
iko imara katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wastaafu na
wanachama wake wote popote pale nchini. “Mafao yenu yapo wastaafu wote,
nendeni mkahakik taarifai, na hata ndugu ambao ndugu zao wastaafu ni
wagonjwa wafike kwenye ofisi zetu na sisi tutakwenda kufanya uhakiki
huko huko aliko.” Alifafanua Bi. Enice Chiume ambaye anaendelea na ziara
yake Jumatano Juni 12, 2019.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

No comments :
Post a Comment