![]() |
| Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe, akikata utepe mara baada ya kuzindua Cliniki ya Kutibu watoto wenye matatizo ya Mguu Kifundo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma |
Baadhi ya Viongozi wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania wakiwa wamebeba mabango katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Madaktari wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania wakiwa katika matembezi ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Daktari bingwa na mbobezi wa
mifupa na viungo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Dkt . Robert Mhina
akizungumza na baadhi ya akina mama wenye watoto wenye ulemavu wa mguu
Kifundo katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo
ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika
jijini Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe ,akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe,akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Bw.Emmanuel Kowero katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe,akitoa maelezo kwa Mratibu Miguu Kifundo kanda ya Kaskazini Bw.Goodluck Pallanayo katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe, akikata utepe mara baada ya kuzindua Cliniki ya Kutibu watoto wenye matatizo ya Mguu Kifundo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma
Daktari bingwa na mbobezi wa
mifupa na viungo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Dkt . Robert Mhina akiagana
na Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe, baada ya kuzindua
Cliniki ya Kutibu watoto wenye matatizo ya Mguu Kifundo katika Hospitali
ya Rufaa Mkoa wa Dodoma
Daktari Bingwa Upasuaji Mifupa Hospitali ya Bugando akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
...................................
NA MWAANDISHI WETU, DODOMA
MGANGA Mkuu Hospitali
ya Rufaa Mkoa, Dodoma Dkt.James Kiologwe amewaomba wazazi /walezi pamoja na
wananchi kutowafungia ndani watoto wenye matatizo ya mguu kifundo.
Watanzania wameungana
na mataifa mengine Duniani katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mtoto
mwenye matatizo ya Mguu Kifundo ambapo zaidi ya watoto elfu mbili mia tano nchi
nzima hugundulika kuwa na tatizo la ulemavu wa mguu kifundo kila mwaka hapa nchini.
Akizungumza katika
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo
yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma Sambamba na Ufunguzi wa Cliniki ya kutibu
Dkt.Kiologwe amesema kuwa jamii inatakiwa kubadilika na kuacha tabia ya
kuwaficha na kuwanyanyapaa watoto wenye Ulemavu huo.
Aidha amewapongeza
wakina mama walioitikia wito na kupeleka watoto wao wenye changamoto ya mguu
kifundo, pamoja na wadau waliodhamini maadhimisho hayo ikiwemo TCCO kwa
kuchagua mkoa wa Dodoma kama sehemu yakwanza kuadhimisha maadhimisho ya watoto
wenye ulemavu wa mguu kifundo.
Pamoja na hayo
amepongeza taasisi mbalimbali kwa kushirikiana na TCCO, kwani wamesaidia
kuwaondolea adha watoto pamoja na vijana ambao walikuwa wanaishi kwenye
mazingira ya unyanyapaa lakini wafadhili kwa kushirikiana na TCCO pamoja na
wadau mbalimbali wamerejesha heshima ya utu wa mwanadamu.
Ameongeza kuwa TCCO
imeshahudumia watu zaidi ya elf nne, ambao wamefanyiwa marekebisho ambapo ni
watanzania wengi wamerejeshewa heshima yao ya utu pamoja na mwonekano.
“ Pongezi nyingi ni
kwaajili ya nia iliyomo mioyoni mwetu lakini nilikuwa nawaambia watu kazi ya
utabibu ni zaidi ya kazi ya uaskofu na nizaidi ya kazi ya upadre sisi
tunamwangalia mtu kwa ujumla wake” amesema Dkt. Kiologwe
Pia Dkt. Kiologwe ameeleza
kuwa thamana waliopewa matatibu ni kubwa kwani kuanzia kuzaliwa mpaka kufa kwa
mwanadamu Daktari pekee ndiyo mwenye kutekeleza shughuli zote hizo hata pale
inapohitajika kumrekebisha madaktari hufanya hivyo pia wanawashukuru wote
waliojitokeza kushiriki maadhimisho hayo.
Aidha amesema kuwa
TCCO wanajumla ya matawi 35 kote nchini (kliniki), ambapo Dkt. Kiologwe ameomba
taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbali mbali kuanzisha kliniki kwenye
kila mkoa na wilaya kwani takribani katika kila watoto elf moja wanaozaliwa
mtoto mmoja anazaliwa na mguu kifundo.
Awali akizungumza
amesema kuwa changamoto ya ufanisi imekuwa tatizo kubwa sana kwa watoto wenye
ulemavu wa mguu kifundo hasa kwenye utendaji wa kazi, elimu, kushiriki kwenye
masuala ya uchumi pia adha ya kuishi kwenye jamii.
Ambapo ni wastani wa
watoto 120, kwa mwaka wanazaliwa kwenye mkoa wa Dodoma peke yake wakiwa na
ulemavu wa mguu kifundo ikiwa ni pamoja na kukumbana na adha ya kwenda kwenye
matibabu ambapo watu wengi wamezoea masuala yote yanayohitaji marekebisho
yanafanyika kwenye hospitali ya CCBRT, ambayo pia ni msaada mkubwa katika nchi
kwani elimu kuhusu wapi matibabu ya ulemavu wa mguu kifundo yanapatikana hivyo
elimu yakutosha inatakiwa kutolewa kwa umma ili kujua ni wapi matibabu ya ulemavu
wa mguu kifundo yanapatikana.
Pia ameeleza
changamoto ambazo zinapelekea watu kushindwa kupata matibabu hayo ni pamoja na
kipato, ambapo kwa uzinduzi wa kliniki hiyo ya marekebisho ya mguu kifundo
yatakuwa yanafanyika kila alhamisi na kwa watoto wote chini ya umri wa miaka
mitano matibabu yatakuwa bure.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Muungano wa Wadau wanaojihusisha na Matibabu ya Mguu Kifundo
Tanzania Dkt.Robert Mhina amesema kuwa bado kuna changamoto miongoni mwa jamii
wakihusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina ambapo amesema wanaendelea
kutoa Elimu kwa jamii ili iache kuwanyanyapaa watoto wenye matatizo ya Mguu
Kifundo.
''Rai yangu kwa
wazazi/walezi pamoja na wananchi kiujumla waache kuwafungia na kuwaficha watoto
wenye ulemavu kwani tatizo hilo linaponyeka hivyo jamii iache tabia ya
kuwanyanyapaa pamoja na kuhusisha ugonjwa huu kwa imani za kishirikina''amesema
Dkt.Mhina
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti baadhi ya Wazazi wenye watoto wenye matatizo ya mguu Kifundo
wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo unyanyapaa miongoni
mwa jamii hivyo wameiomba Serikali kufanya msko na kuwachukulia hatua baadhi ya
wazazi wanaowaficha watoto wenye matatizo hayo ya Ulemavu
wananchi kutowafungia ndani watoto wenye matatizo ya mguu kifundo.






No comments :
Post a Comment