Saturday, June 29, 2019

DPP AKABIDHI MADINI, VITO NA FEDHA BENKI KUU (BOT) ZILIZOTOKANA NA KESI ZA UHUJUMU UCHUMI. JUNI 29,2019

  Masanduku yaliyoifadhiwa Madini,Vito pamoja na fedha za Mataifa mbalimbali zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi zikiingizwa Ukumbini tayari kwa Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga kukabidhi kwa Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali  sehemu ya vipande vya Madini ya Dhahabu ambayo ilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria  zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 20
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt.Agustine Mahiga, Waziri wa Madini Dotto Biteko pamoja na Kamishina wa Madini Profesa Abdukalim Mruma wakiwa wamishika vipande vya madini ya dhahabu ambayo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amezikabidhi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali Madini, vito na Fedha za mataifa mbalimbali zilizokamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria  zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019

No comments :

Post a Comment