
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Itembe Akizungumza na waandishi wa
habari katika uzinduzi wa kampeni ya Amsha Ndoto ‘Amsha Ndoto’ yenye
lengo la kuwahamasisha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na
utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kuwa na maisha ya baadaye yaliyo
imara kifedha.Kulia kwake ni Mkurungezi wa Biashara wa Benki ya Azania
Rhimo Nyansaho na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Uendeshaji wa Azania
Bank, Jane Chinamo mapema leo Jijini Dar es salaam.
***
Benki
ya Azania (ABL) imetangaza uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina, ‘Amsha
Ndoto’ yenye lengo la kuwahamasisha wateja wake na watanzania kwa ujumla
kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kuwa na maisha ya baadaye
yaliyo imara kifedha.
Kampeni
itaendeshwa kwa miezi mitatu, kuanzia 27 Juni 2019 hadi 27 Septemba
2019 na itahusisha wateja wa zamani na wapya ikijikita zaidi katika
bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti(kwa ajili ya
kila mmoja) na Watoto Akaunti(kwa ajili ya watoto tu).
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa ABL, Charles Itembe, Ili kustahili
kupokea zawadi, wateja wanapaswa kuwa na akiba yenye thamani ya TZS
1,000,000 kwenye akaunti zao na kuendelea ili kuwawezesha kustahili
kuingia kwenye fainali ya droo na hatimaye kuweza kushinda. Washindi wa 3
watapatikana kila mwezi. Kupitia kampeni hii wateja wataweza
kujishindia mpaka mara mbili ya kiwango walichoweka kwenye akaunti,
ambapo kiwango hiki cha zawadi huweza kufikia mpaka Shilingi milioni
Tatu
Akiongelea
kuhusu vigezo vya washiriki, Itembe alisema kuwa wateja ni lazima
waweke akiba ya kiasi cha TZS 500,000 6% katika kipindi chote cha
kampeni na mwaka mzima, na wale watakaoweka akiba kiasi cha TZ 1,000,000
watapewa tokeni zitakazowawezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho
itakayowapata washindi.
“Tunawahamasisha
watanzania wote, wateja wetu wa sasa na wapya,wazazi na walezi kufungua
akaunti hizi ili kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo
salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafuta namna gani ya kuongeza
mitaji, kulipia kodi za pango na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya
baadaye”, alisema Itembe, akigusia pia kuwa akaunti hizi zitakuwa fursa
ya kuwahimiza kuweka akiba kwa ajili ya .
Promosheni hii, yenye kaulimbiu: ‘Weka Akiba Ushinde,tumuwezeshe ada ya shule’,
itawasilishwa kupitia radio na mitandao ya kijamii kama Facebook,
Instagram, Twitter, LinkedIn, Google Display placement na tovuti za
ndani. ABL pia imetengeneza tovuti ndogo kwa wateja wapya kujiunga na
inaweza kupatikana kupitia linki hii: amshandoto.com.
Masharti na vigezo kuzingatiwa
No comments :
Post a Comment