Shirika
la Ndege la Tanzania (ATCL), leo limeanza rasmi safari yake ya kwanza
kuelekea Johannesburg, Afrika Kusini kwa kutumia ndege aina ya Airbus.
Mkurugenzi wa Shirika hilo Mhandisi Ladslaus Matindi amesema kwa wiki kutakuwa na safari nne.
Ndege
hiyo aina ya Airbus 220-300 imeondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Dar es Salaam Tanzania (JNIA) saa 4:30 asubuhi
ikitarajia kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa OR Tambo, Afrika Kusini
saa 6:45 mchana.

No comments :
Post a Comment