Na Paschal Dotto-MAELEZO
Ni
Takribani Miaka 120 ambapo historia iliandikwa, mwaka 1912, Serikali ya
Kikoloni nchini iliamua kuimarisha sekta ya usafirishaji Kwa kujenga
Reli, ambapo njia zake ziliunganisha Miji hasa maeneo ya kilimo,
uzalishaji na kibiashara, reli kuu kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza,
hatimaye Kigoma na Tanga.
Ni
dhahiri sasa tunaona Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
akifanya mageuzi makubwa Kwa kujenga reli ya kisasa, maarufu SGR
(Standard Gauge Railway) ambapo kwa vyovyote tutasogeza nyuma zaidi
kuhusu historia ya reli nchini, kwani Rais anatakeleza Ujenzi wa Reli ya
Kisasa, Standard Gauge Railway (SGR) kwa maslahi makubwa kiuchumi.
Katika
hafla ya uwekaji wa Jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya SGR awamu ya
pili, Morogoro-Makutupola, iliyofanyika 14, Machi, 2018, Rais Magufuli
aliwakumbusha Watanzania kuwa Tanzania imekuwa nchi ya pekee Barani
Afrika katika kutekeleza mradi huo mkubwa kwa pesa za walipa kodi wake.
“Kwa
bahati nzuri, hivi karibuni tulitembelewa na Rais wa Uturuki, Recep
Tayyip Erdogan, na alishuhudia kwamba Tanzania tumetayarisha fedha zetu
wenyewe, kwa nguvu zetu wenyewe, na walipa kodi ni watanzania wenyewe,
Tsh Trilioni 2.8 na kutangaza tenda zilizokuwa wazi, makampuni zaidi ya
40 yalijitokeza kuwania tenda, na bahati nzuri kampuni kutoka Uturuki
ikashinda tenda hii,” alisema Rais Magufuli na kuongeza kuwa Uturuki
itatupa mkopo wa masharti nafuu kwa awamu zingine za ujenzi, Rais
akaongeza, “ kwa hiyo Tanzania tunaweza”,
Rais
Magufuli aliwataka watanzania kutambua fursa za upitapo mradi wa SGR na
kuwataka wafanyabiashara wakubwa, wadogowadogo, mama ntilie, kunufaika
wakati wa ujenzi na mara baada ya ujenzi, na kwamba itakuwa nguzo kubwa
kwa usafarishaji kwenye maeneo hayo na nchi nzima.
“Katika
uchumi wa nchi yoyote duniani, Sekta ya Usafirishaji ni muhimu sana,
kwa hiyo Serikali kuchukua hatua madhubuti ya kuimarisha sekta ya
usafirishaji kwa kujenga reli ya kisasa, SGR, ni moja ya Mwarobaini wa
kutatua changamoto ya usafirishaji mizigo na kulinda usalama wa
barabara”. Alisikika mmoja wa wahandisi akiwaeleza waliowatembelea.
Mageuzi
ya Rais Magufuli yanalenga kuwaimarisha wananchi, si tu wafanyabiashara
bali hata wasafiri kwa utekelezaji wa ujenzi wa Reli ya kisasa, SGR
yenye kasi ya 160km/saa utakuwa na faida kuwabwa kwani masaa 2.5 Dar es
Salaam-Morogoro na masaa tisa kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ni
dhahiri kutakuwa na Furaha kubwa kwa watu kuwahi kufika Mwanza mapema
badala ya saa saba usiku au kulala Shinyanga.
“Ujenzi
wa Reli hii (SGR), kwa Tanzania siyo chaguo bali ni lazima, kwani hatua
hii ilitakiwa ifikiwe zamani, lakini sasa Rais Magufuli ameamua
kutufikisha kwenye teknolojia mpya katika sekta ya usafirishaji, kwani
matatizo mengi ya barabara yanatokea kwababu ya mizigo mizito, hakuna
reli imara ya kubeba mizigo hiyo, kwa hiyo ujenzi wa Reli hii ni maamuzi
sahihi kwa Serikali yetu.”, Anaeleza Mkurugenzi TRC, Masanja Kadogosa.
Kadogosa
anasema, Reli hiyo ambayo inatumia nishati ya umeme imekuja wakati
mwafaka ikiwa Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa
Mto Rufiji (Rufiji Hydroelectric Power), wenye kutoa Megawati 2,115, kwa
hiyo treni hiyo itapata umeme wa kutosha.
“SGR,
Ni mradi mkubwa ambao unatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini
ya Rais Magufulu kwa kutumia fedha za walipa kodi wake kwahiyo ni vyema
watu wakafahamu kuwa kodi yao inaenda wapi Trilioni 7 siyo mchezo”,
alisema Kadogosa.
Ili
kutekeleza adhima ya kuutangaza mradi huo kwa wananchi, Mei 17, 2019,
Jopo la Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri
pamoja na Makatibu Tawala takribani 400 wakiongozwa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Seleman Jafo walitembelea kuona mradi huo ili
kupeleka ujumbe kwa wananchi.
Kabla
ya Safari hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa aliwapitisha
kidogo wageni wake katika shule ndogo kuhusu mradi ili kutambua umuhimu
wa Mradi huo kwenye sekta ya usafirishaji na kwa wananchi.
Masanja
alieleza kuwa Reli hiyo inayojengwa inaenda kufuta zana
mbalimbaliikiwemo ile historia ya kikoloni, kuwa reli iliyopo ilijengwa
na wakoloni, lakini pia ujenzi wa Reli hiyo sasa unaenda kuimarisha
sekta ya usafirishaji. Serikali inatekeleza ujenzi huo Kwa Kipande cha
Dar es Salaam-Morogoro, Morogoro-Makutupola na badae kutekeleza ujenzi
huo hadi Mwanza, kilometa 1,219.
Kadogosa
alisema kuwa Reli hiyo, SGR inauwezo wa kubeba tani milioni, 10,000,
kwa mkupuo sawa na malori 500 yenye tani 20, Treni tano zenye tani
10,000 na kuwa na kasi kubwa ya 160km/saa, tofauti na ya sasa ambayo
inakasi ya 30km/saa, kwa Afrika itakuwa ni Reli pekee yenye uwezo mkubwa
kama huo, tani Miliomi 10-17 zitasafirishwa kwa mwaka, kwa hiyo SGR ni
mwamba sekta ya usafirishaji nchini.
Aidha,
Kadogosa alieleza kuwa ujenzi wa Reli (SGR), Dar es Salaam-Morogoro
unatekelezwa na Kampuni kutoka Uturuki, Yapi Merkezi takribani Trilioni
2.7, lakini kwa sehemu nyingine ni Yapi Merkezi na Portuguese
Construction Group Motel-Engil.
kukamilika
kwa mradi huo kutakuwa na ufanisi mkubwa kwenye sekta ya usafirishaji
nchini kwa kubeba mizigo tani nyingi lakini pia kasi yake katika
kusafirisha abiria, kutoka Dar es Salaam- Dodoma treni itakuwa inafanya
safari mara nane kwa siku, kwa hiyo ni hatua kubwa kwa sekta ya
usafirishaji.
Kadogosa
alizitaja baadhi ya Faida za Mradi huo Kwa sasa kwa wananchi na uchumi
wa nchi kwa ujumla kwani kwa sasa watanzania walioko sehemu za ujenzi
wanafaidika na kupeleka malighafi za ujenzi, mama ntilie kupika chakula
na biashara zingine.
“Takribani
mifuko ya simenti milioni, 9,200,000 ambayo ni sawa na tani 600, nondo
kilo milioni 115 sawa na tani 1500 na mataluma 1,400,000, kutoka kwa
wasambazaji wa malighafi hizo takribani 500, wafanyakazi 10, 000, huku
asilimia 94 ya wafanyakzi hao ni watanzania, pia asilimia 48 ya wataalam
ni watanzania, kwa hiyo pamoja na mradi huu kuwa nguzo imara ya
usafirishaji nchini, SGR imekuja kutoa Fursa za ajira kwa watanzania”,
Alisema Kadogosa.
Kadogosa
alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na uwezo wake ni wa juu, na sasa
matatizo ya usafarishaji nchini yatapata suluhu kubwa, kuimarisha na
kulinda barabara nchini.
Katika
sekta ya usafirishaji wa mizigo hasa ile mikubwa inayotoka bandarini
kwenda sehemu zingine za nchi na mengine nje ya nchi, kwani kuwepo kwa
Reli imara itasababisha utendaji kazi wa bandari kuwa na ufanisi mkubwa,
“Bandari inategemea kuwepo kwa miundombinu imara kwa upande wa nchi
kavu, hakuna ufanisi wa Bandari bila kuwa na Reli imara, Serikali
imeliona hilo ndiyo maana ikaamua kutekeleza haraka ujenzi wa Reli ya
Kisasa (SGR) na Reli yetu hii inabeba mizigo mingi Takribani Tani
Milioni 17 kwa mwaka, hakuna Reli kama hii Barani Afrika” Kadogosa.
No comments :
Post a Comment