Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
Tanzania
imetajwa kuweka historia katika tasnia ya madini baada ya Almasi yenye
Karati 512.15 kupatikana hivi karibuni katika eneo la Maganzo Mkoani
Shinyanga na kuuzwa kwa jumla ya shilingi Bilioni 3.2.
Akizungumza
katika mahojiano maalum kuhusiana na madini hayo,Naibu Waziri wa
Madini Mhe. Stanslaus Nyongo amesema kuwa kutokana na kupatikana kwa
almasi hiyo Serikali itapata mapato ya takribani shilingi milioni
235,000/- kama kodi na tozo mbalimbali ikiwemo mrabaha ambayo yamelipwa
Serikalini baada ya mauzo hayo.
Kuuzwa
kwa jiwe hilo moja la almasi katika soko la madini mkoani Shinyanga ni
muendelezo wa tija inayopatikana kupitia masoko hayo toka kuanzishwa
kwake nchini,jumla ya shilingi bilioni 34.3 zimepatikana kwenye biashara
ya dhahabu iliyofanyika katika kipindi cha mwezi mmoja tu kati ya Machi
17 mpaka Aprili 17 mwaka huu katika masoko ya madini kote nchini, kwa
mujibu waziri wa Madini,Doto Biteko, aliyetoa taarifa hiyo hivi
karibuni.
“Natoa
wito kwa wachimbaji wote,madalali na mawakala,kuyatumia ipasavyo masoko
hayo kwakuwa kila mmoja atapata stahiki yake tofauti na awali kabla ya
kufunguliwa kwa masoko hayo ambapo wachimbaji hawakuwa kwenye mikono
salama kufutia kutokuwa na mfumo rasmi wa uuzaji madini yao”.Alisisitiza
mhe. Nyongo
Akifafanua
amesema kuwa kila mchimbaji anapaswa kuzingatia sheria na Kanuni za
sekta ya madini ili kuepuka mkono wa sheria na hatua nyingine ikiwa ni
pamoja na kutaifishwa kwa madini yao pale watakapobainika kutaka
kutorosha madini ama kujihusisha na magendo.
Aliongeza
kuwa baada ya kupatikana kwa almasi hiyo wataalamu wa Wizara hiyo
walifanya tathmini ili kuona ubora wake na kiwango kilichopatikana ili
kuhakikisha kuwa Serikali inapata mapato yake.
“
Serikali ya Awamu ya Tano imeweka makazo katika kuimarisha sekta ya
madini nchini ili itoe mchango unaostahili katika uchumi wetu ndio maana
tunaona kuwa kupitia masoko ya madini tuliyoanzisha hata mchimbaji huyu
aliyepata hii almasi pale Maganzo aliiuza kupitia soko letu la madini
baada ya kufuata taratibu zote” alisisitiza Mhe. Nyongo
Tanzani ni moja ya nchi zenye utajiri mkubwa wa madini ya aina mbalimbali ikiwemo Almasi, Tanzanite, Dhahabu na mengine mengi.
Serikali
ya Awamu ya Tano imeweka mkazo katika kuimarisha sekta ya madini
ikiwemo kuimarisha taratibu za uuzaji wa madini yote yanayozalishwa hapa
nchini, kuimarisha usimamizi, kuwawezsha wachimbaji wadogo ili waweze
kuchimba kwa tija.
No comments :
Post a Comment