Monday, May 27, 2019

Mama aliyekamatwa Uhamiaji Marekani azuiwa kumzika mwanaye


Kufuatia vizuizi vilivyowekwa na Serikali ya Marekani kwenye mpaka baina yao na nchi ya Mexico mwezi Disemba mwaka jana, hadi sasa takribani watoto sita wamepoteza maisha wakiwa kizuizini chini ya uangalizi wa maofisa uhamiaji wa Marekani. Leo mtoto mdogo zaidi kati ya waliopoteza maisha, Wilmer Josue mwenye umri wa miaka miwili na
nusu amezikwa na nduguzake baada ya kufariki Mei 14, kizuizini na mama yake mzazi hajaruhusiwa kutoka chini ya ulinzi wa maofisa uhamiaji kwenda kumzika kijijini kwao Olapa.
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na mtaalamu wa afya aliye mhudumia mtoto huyo alipofikishwa kituo cha Afya kabla hajafariki, amesema kuwa mtoto huyo alikutwa na ugonjwa wa Nimonia.
Jirani wa karibu wa mama aliyempoteza mtoto Wilmer ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa mama huyo aliamua kwenda Marekani ili kumsaidia mwanae ambaye alikuwa anahitaji matunzo maalumu kwa maradhi aliyokuwa nayo na yeye hakuwa na fedha za matibabu.
Kifo cha mtoto Wilmer kimefuatia miezi mitano baada ya mtoto wa Guatemalan kufariki mpakani hapo, mwezi disemba mtoto wa miaka saba Jakelin Caal alifariki pia mikononi mwa polisi wa mpakani hapo.
Zaidi ya watu 300,000 walizuiliwa kwenye mpaka wa Marekani na Mexico tokea Januari hadi Aprili mwaka huu, na bado idadi ya wahamiaji wanaotaka kupita mpaka huo inaongezeka kila mwezi.
Uongozi wa Marekani umesema kuwa hauna vifaa vya matunzo kwa wahamiaji haramu kwa wanaoendelea kuongezeka mpakani hapo na ongezeko la wahamiaji haramu kukwama mpakani limekuja baada ya Rais Donald Trump kuapa kukomesha uhamiaji haramu katika mipaka ya Marekani na Mexico.

No comments :

Post a Comment