Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro, akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo la Ushirika, Tukuyu
mkoani Mbeya leo, wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi katika wilaya za
Rungwe na Kyela mkoani humo ambapo IGP Sirro aliwataka wananchi
kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwafichua wahalifu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro, akinunua matunda kutoka kwa mmoja wa wajasiliamali katika eneo la
Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi
katika wilaya za Rungwe na Kyela mkoani humo kwa lengo la kuona
utendajikazi unaofanywa na askari wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro, akizungumza jambo na mmoja kati ya wajasiliamali ndogo ndogo
katika eneo la Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, IGP Sirro yupo mkoani
hapa kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Claudia Kitta,
wakati alipowasilia wilayani humo kwa ziara ya kikazi yeye lengo la
kuona utendajikazi unaofanywa na askari wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la
Polisi.
No comments :
Post a Comment