Ahadi hiyo ilitolewa jana na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NMB Albert Jonkergouw katika hafla fupi ya
benki hiyo kwa taasisi za serikali, viongozi wa taasisi na
wafanyabiashara iliyofanyika katika ukumbi wa new Dodoma
hotel.Mkurugenzi huyo alisema nguvu kubwa imeelekezwa kwa wakulima
kutokana na sera ya Tanzania ya viwanda lakini akasifu mpango wa
serikali kuhamia Dodoma ambao umeungwa mkono na benki hiyo.
Jonkergouw alisema katika kuunga
mkono uhamiaji Dodoma, NMB wameshapeleka tawi la benki tembezi katika
mji wa kiserikali Mtumba na kwamba mipango ya baadae ni kufanya
maboresho makubwa ya huduma za benki katika eneo hilo.
“Tutaendelea kuunga mkono juhudi
za serikali kwa kila hali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wakulima na
wafanyabiashara, mimi niseme kuwa benki hii ni mali yenu mna haki ya
kuitumia nasi ni wajibu wetu kuwahudumia,” alisema Mkurugenzi.
Akizungumza katika halfa hiyo,
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge aliomba uongozi wa NMB
kuutazama mkoa wa Dodoma kwa jicho la pekee kutokana na ongezeko la watu
kufuatia ujio wa makao makuu.
Dk Mahenge aliomba benki
kurahisisha masharti katika upatikanaji wa mikopo ikiwemo kuwapa
kipaumbele zaidi wakulima wa zabibu zao linalotajwa kuwa mkombozi kwa
wenyeji w amkoa huo.
Mkurugenzi wa hospitali ya
Benjamini Mkapa ya Jijini hapa Dk Alfonce Chandika alisema benki ya NMB
ni rafiki kwa makundi yote kutokana na huduma zake kuyagusa makundi
yote.
Dk Chandika alisema kwa sasa
huduma zinazotolewa na benki hiyo zinapaswa kuwa mfano kwa taasisi
zingine jambo litakalotoa tafsiri chanya kwa Tanzania ya viwanda.
Mkurugenzi wa Benki ya NMB –
Albert Jonkergouw akiongea na watumishi wa Serikali na wafanyabiashara
kwenye chai ya Asubuhi iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwaajili ya
kuelezea utayari wa Benki hiyo katika kuhudumia Serikali jijini Dodoma
jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DR.
Binilith Mahenge (Kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya NMB –
Albert Jonkergouw (Kulia) kwenye chai ya Asubuhi iliyo andaliwa na Benki
ya NMB kwaajili ya kuelezea utayari wa Benki hiyo katika kuhudumia
Serikali jijini Dodoma jana.
No comments :
Post a Comment