Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa
Wateja wa Tigo Mwangaza Matotola, akiwaonyesha waandishi wa habari
(hawapo pichani) namna ambavyo huduma ya WhatsApp inavyoweza kutumiwa na
mteja kuuliza au kupata ufafanuzi kutoka kwa watoa huduma wa Tigo.
Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tigo Woinde Shisael
Meneja Mawasiliano wa Tigo Woinde
Shisael (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa
uzinduzi wa huduma ya WhatsApp ambayo inaweza kutumiwa na wateja wa
kampuni hiyo kuuuliza au kupata ufafanuzi wa bidhaa na huduma mbali
mbali za kampuni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja
cha Tigo Mwangaza Matotola
Baadhi ya waandishi wa habari
wakiuliza maswali wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya WhatsApp ambayo
inaweza kutumiwa na wateja wa Tigo kupata ufafanuzi au kutatuliwa
changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo wakati wakitumia mtandao wa
Tigo.
…………………………..
Mwandishi Wetu
Kampuni ya Tigo Tanzania, leo imezindua huduma ya whatsApp kwa ajili ya kuwahudumia wateja wake.
Huduma hii ya kidijitali,
itawawezesha wateja wa Tigo kutuma dukuduku zao na kupokea
majibu ya
papo kwa papo watakapotumia namba ya WhatsApp ambayo ni 0675100100.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
huduma hiyo mpya jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Huduma
kwa Wateja wa Tigo Mwangaza Matotola alisema, Tigo imekuwa kampuni ya
kwanza nchini kutumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp kuwahudumia wateja
wake.
“Kupitia huduma hii mpya, wateja
wa Tigo watapata uzoefu binafsi pamoja na kupata majibu ya papo kwa papo
watapotaka kupata ufafanuzi wa jambo au utatuzi wa changamoto zozote
katika kutuia mtandao wetu,” alisema
WhatsApp ni moja kati ya mitandao
ya kijamii yenye nguvu sana duniani kwa sasa. “Kwa kuzingatia ukweli
huu, huduma hii itawawezesha wateja wa Tigo kupata huduma binafsi na
zenye usalama. Uzinduzi wa huduma hii ni moja kati ya mikakati yetu ya
kuhamasisha maisha ya kidijitali, vile vile tunapanua wigo wa namna
wateja wetu wanavyoweza kuhudumiwa tunavyoongeza WhatsApp kwenye huduma
zetu za mitandaoa ya kijamii kama Facebook, Instagram na Twitter. Huduma
ya WhatsApp inapitakana kwa wateja wote wa Tigo,” alifafanua Mwangaza.
Mwangaza aliongeza kuwa, huduma
hiyo imetengenezwa maalum kwa ajili ya kumhudumia mtu mmoja mmoja na
siyo kuwahudumai watu kwa pamoja kama kundi (group la WhatsApp). “Mteja
siyo tu ataweza kujielezea kupitia huduma hii lakini pia anaweza kutuma
picha kwenye mfumo wa ‘screenshot’ kwenda namba 0675100100 na atapata
majibu ya papo kwa papo kwa kile atachoakiuliza au kutaka
ufafanunuzi/utatuzi,” alisema.
“Tigo Tanzania inajivunia kuwa
kampuni ya simu namba moja kwenye mageuzi ya kidijitali pamoja na
uvumbuzi. Tigo imeweza kuwa ya kwanza kuzindua bidhaa nyingi kwenye soko
la Tanzania ambazo zinathibitisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora kwa
wateja wetu pamoja na uzoefu wa aina yake. huduma hii ya WhatsApp ni
sehemu ya safari yetu hii ya mageuzi ya kidijitali,” aliongeza
Wateja wanaotumia WhatsApp
wanaweza kuwasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja cha Tigo muda
wowote wanaopenda na kama itatokea kukawa na kuchelewa kupata mrejesho
atapokea ujumbe mfupi.
Huduma hii mpya ya WhatsApp
kwa ajili ya kuwahuduma wateja, ni sehemu ya mkakati wa kampuni ya Tigo
kuwapatia wateja wake uzoefu wa aina yake na wa kipekee wa huduma zake
kwa njia ya kidijitali na kurahisisha maisha yao ya kila siku kupitia
huduma zilizojaa ubunifu.
No comments :
Post a Comment