Kiongozi wa timu ya 28 ya
Madaktari kutoka China (kushoto) Dkt. Zhang Zhen akitoa taarifa kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maendeleo ya matibabu
Duniani ambayo hivi sasa yanafanyika pia katika Hospitali ya Mnazimmoja
kupitia madaktari wa China kwa mashirikiano na madaktari wazalendo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya
kiharusi kutoka China Mlao Xingi akizungumza na wandishi wa habari juu
ya mafanikio aliyoyapata katika kutoa tiba kwa wagonjwa wa maradhi hayo
kwa kutumia sindano za chuku (Acupuncture).
Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti
Wizara ya Afya Zanzibar Mwinyi Msellem (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya madaktari wa China na waandishi wa habari.
Picha na Makame Mshenga.
………………..
Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na
Madaktari bingwa kutoka China imewataka wananchi kwenda hospitali ya
Mnazi Mmoja kupata huduma muhimu za matibabu ya maradhi ya
Mkojo na
matatizo ya mishipa ya hisia bila ya malipo.
Akizungumza na waandishi wa
habari, Mkurugenzi Mafunzo na Utafiti Wizara ya Afya Mwinyi Mselem
amesema huduma za maradhi hayo zinatolewa katika Hospitali ya Mnazimmoja
na hakuna haja ya kufuatilia matibabu nje ya nchi.
Amesema timu ya madaktari bingwa
kutoka China wamefanikiwa kutoa huduma za matibabu ya maradhi ya Mkojo,
uvimbe mkubwa na matatizo ya mishipa ya hisia (kiharusi) na wagonjwa hao
wanaendelea vizuri.
“Kulikuwa na mgonjwa ana saratani
na tatizo la haja kubwa madaktari wa kichina walimfanyia upasuaji na
kuweza kuondoa tatizo pia kwa kutumia njia ya adpancha wameweza kumtibu
mgonjwa aliyekuwa hana hisia ambae hawezi kuzungumza na wafanikiwa na
sasa anaendelea vizuri”, alieleza Mkurugenzi huyo
Mkurugenzi Mwinyi amewataka
wananchi kuiamini hospitali ya rufaa ya Mnazi mmoja kwa vile huduma zake
zimeboreshwa sana na wagonjwa ambao matatizo yao yameshindikana katika
vituo vidogo vya afya kuitumia hospitali hiyo.
Nae Kiongozi wa timu ya Madaktari
hao Dk. Zhang Zhen amesema wamefanikiwa kufanya matibabu ya maradhi
mbali mbali yaliyokuwa yakionekana hayawezi kutibika Zanzibar.
Amesema timu hiyo imeanzisha
Upasuaji kwa kutumia njia ya matundu kuondosha tatizo la Tezi Dume bila
ya kupasua sehemu kubwa ambayo ni nzuri na rahisi katika kutoa huduma za
mardhi ya aina hiyo.
Timu ya 28 ya madaktari kutoka
China yenye madaktari 18 wataendelea kuwepo Zanzibar hadi mwezi Julai
mwaka huu na wanatoa huduma katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja na
Abdalla Mzee Mkoani na wanasaidia vituo vyengine vya Afya Unguja na
Pemba.
No comments :
Post a Comment