Waziri wa Nishati Mhe . Dkt Medard
Kalemani akizindua Mradi wa uunganishwaji umeme vijijini Katika kijiji
cha Osteti kata ya Chapakazi Wilayani Kiteto Mkoa wa Manyara .
Mhe. Dkt. Medard Kalemani
akizungumza na mafundi wanao endelea kuunganishia umeme wateja wa Kijiji
cha Osteti kilichopo kata ya Chapakazi wilayani Kiteto Mkoani Manyara ,
ambapo Mhe. Dkt Medard kalemani alizundua mradi wa umeme vijijini
katika kijiji hicho leo 25 April 2019
Mhe. Dkt Medard Kalemani
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Dosidosi kata ya Dosidosi alipo
washa umeme kwa Mara ya kwanza katika Shule ya Sekondari ya Dosidosi,
Dosidosi ni Miongoni mwa vijiji 47 vinavyo nufaika na Mradi wa umeme
vijijini awamu ya tatu (REA III) Wilayani Kiteto Mkoa wa Manyar
………………..
Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa
uunganishwaji umeme vijijini katika Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara,
Akizungumza na
wanaichi wa Kijiji cha Dosidosi Mhe. Waziri alisema,
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imedhamiria kupeleka umeme katika
kila kijiji nchini kwa kupitia miradi inayo endelea ya umeme vijijini
, Utekelezaji huu unalenga kuifikia azma yaa Serikali ya kuwapatia
umeme wananchi wote wa vijiji ifikapo mwaka 2025.
Katika ziara hiyo Mhe. Dkt
Kalemani aliwahakikishia wanavijiji vya Orgine,Soweto,Esukita,Kibaya,
Azimio, Osteti pamoja na Dosidosi kuwa ifikapo Mwezi Septemba 2019
wanavijiji hao pamoja na vijiji vingine 47 vya wilaya ya Kiteto
watakuwawamekwisha washiwa umeme, Mhe. Waziri pia alitumia hadhira hii
kutoa maagizo kwa Mameneja wote wa TANESCO, Kuhakikisha wanawaunganishia
umeme wateja wote walio lipia hadi tarehe 31 mwezi wa tatu, Mhe. Waziri
pia alisisitiza Wananchi kulipia kwa wingi ili waweze kunufaika naa
fursa ya kuunganishiwa umeme kwa gharama nafuu ya shilingi Elfu 27000
tu.
Naye Mbunge wa Kiteto Bwana Emily
Papian alimshukuru Mhe .Waziri wa Nishati kwa kuzindua Utekelezaji aa
Miradi ya umeme vijijini katika jimbo la Kiteto pia kwa kutoa Vifaa
vya Umeta 250 vitakavyogawiwa kwa wananchi ambao hawata weza kufanya
“wirering”katika nyumba zao ili waweze kuunganishiwa huduma ya umeme.
No comments :
Post a Comment