Tuesday, April 2, 2019

Wataalamu wa Ulinzi na Usalama wa vyanzo vya mionzi Afrika Mashariki washiriki Mafunzo jijini Arusha


IMG_1006
Wataalamu 25 wa Ulinzi na Usalama wa vyanzo vya mionzi kutoka katika nchi sita za Afrika wanaoshiriki katika mafunzo ya wiki mbili ya jinsi ya kuendesha mafunzo ya  ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionz katika nchi zao wakiwa katika picha ya pamoja katika Makao Makuu ya Ofisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Jijini Arusha. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kwa ushirikiano na Jumuia ya Umoja wa Ulaya (EU)
IMG_1013 (1)
Wataalamu wa Ulinzi na Usalama wa vyanzo vya mionzi kutoka katika nchi sita za Afrika wanashiriki katika mafunzo ya wiki mbili ya utoaji mafunzo ya ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi yanaoendeshwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa ushirikiano na Jumuia ya Umoja wa Ulaya (EU)
Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano cha Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngamilo amesema kuwa mafunzo hayo yanafanyika katika ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania jijini Arusha na jumla ya washiriki 25 wanashiriki mafunzo hayo kwa kwa lengo la kupata
ujuzi wa namna ya kufundisha wataalamu mbali mbali wanaohusika na ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi katika nchi zao.
Ngamilo amesema kuwa baada ya wakufunzi hao wa ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi kumaliza mafunzo yao watakuwa na uwezo wa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wenzao wa idara mbalimbali za kitaifa katika nchi zao katika kuhakikisha kuwa vyanzo vya mionzi vinatumika katika njia zilizo salama na halali.
“Wakufunzi hawa waliopo kwenye mafunzo wakitoka hapa watakuwa na uwezo wa kuandaa na kufanya mafunzo ya ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi kwa wadau mbalimbali katika nchi zao, pia watatumika kama wataalamu katika kushughulikia matukio yoyote ya maafa ya vyanzo vya mionzi iwapo yatatokea katika nchi za bara la Afrika”alisema Ngamilo.
Hata hivyo amesema kuwa vyanzo vya mionzi visipodhibitiwa vinaweza kutumika katika vitendo vya kigaidi na kuleta madhara makubwa kwa jamii na kuathiri shughuli za kimaendeleo na kiuchumi
Na pia amesema kuwa wakufunzi hao wanajengewa uwezo wa kutoa mafunzo ya kubaini usafirishaji haramu wa vyanzo vya mionzi hasa kwa wataalamu wa mamlaka za ulinzi na usalama ikiwemo Polisi, Walinzi waliopo mipakani na wasimamizi wa Tekinolojia ya Nyuklia, maafisa forodha na wataalamu wa kupambana na majanga ya nyuklia.
Amezitaja metaja nchi wanazotoka washiriki wa mafunzo hayo ni pamoja na Burundi, Uganda, Congo(DRC), Zambia,Ghana na wenyeji Tanzania.

No comments :

Post a Comment