Mratibu
wa TIMUN 2019, Kevin Edward (kulia) akitoa maelezo kuhusu namna vijana
wanavyonufaika na Mkutano wa vijana unaoendeshwa kwa mfumo wa Mikutano
ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
katika ukumbi wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa, nchini Bi Didi Nafisa.
Ofisa
Habari wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi Didi Nafisa akielezea namna
ambavyo vijana wanavyokutanishwa kujadili namna ya kutekeleza vipengele
vya maendeleo endelevu (SDGs) kwa kuwasilisha hoja za kitaifa; na namna
Umoja wa Mataifa unavyosaidia makundi ya vijana kufikia usitawi wakati
wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa YUNA Tanzania, Bw. Jolson Masaki (kushoto) akitoa ushuhuda namna
TIMUN inavyosaidia vijana. TIMUN hufanyika mara moja kwa mwaka na hii ni
TIMUN ya 22. Katika mkutano huo vijana hujadiliana kuhusu mambo
mbalimbali ya duniani na kutoa nafasi ya kupata suluhu yenye ubunifu
mkubwa.
ZAIDI
ya vijana 200 kutoka nchini na nje ya nchi wanatarajia kuhudhuria
mkutano mkubwa utakaoendeshwa kwa mfano wa mfumo wa Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa, kisheria na kikanuni.
Mkutano
huo utakaofanyika Morogoro unatambuliwa kimataifa kama Tanzania
International Model United Nations (TIMUN) unajumuisha vijana kuanzia
miaka 15-30.
Akizungumza
katika mkutano wake na waandishi wa habari, mratibu wa tukio hilo Bw.
Kelvin Edward alisema: “Nimefurahishwa sana kuona washiriki wengi wa
tukio la mwaka huu wanataka kuhakikisha kwamba vijana wa leo na kesho
wanawezeshwa . Nashukuru sana mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
Tanzania kwa kuwezesha jukwaa la vijana kubadilishana mawazo kuhusu
utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu kufikia mwaka 2030. Katika
mkutano huo vijana watapata nafasi ya kubadilisha mawazo na kuelezea
matumaini yao .”
Mkutano
wa mwaka huu utazingatia zaidi kuangalia maendeleo endelevu (SDGs).
majadiliano yatalenga zaidi ushiriki wa vijana katika kipengele cha tatu
cha SDG kinachogusa Afya na ustawi; Kipengele cha nane kazi zenye staha
na ukuaji wa uchumi; kipengele cha 13 mabadiliko ya tabia nchi na
kipengele cha 16 cha amani, haki na taasisi zenye uwezo .
Akizungumza
kwa niaba ya Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa , Msemaji wa umoja huo
kitaifa, Bi. Didi Nafisa amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia
vijana katika utekelezaji wa SDGs. “Vijana wanafanya idadi kubwa ya
wananchi. Ni muhimu kwa wao kupewa taarifa na pia kuhusishwa na
utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu hasa kwa sasa ambapo
kinachoangaliwa zaidi ni matokeo.”
TIMUN
inaendeshwa na Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA), na hufanyika kila
mwaka kwa vijana kuletwa pamoja kutoka mataifa mbalimbali duniani .
Akizungumza
na mwenyekiti wa YUNA Bw. Jolson Msaki amesema matukio kama ya TIMUN
yanaleta vijana karibu na Umoja wa Mataifa na kuongeza uwezo wa vijana
kujadili masuala yanayogusa dunia na kupata fursa ya kutoa suluhu ya
utekelezaji wa SDGs .
Tukio
la mwaka huu limedhaminiwa na Umoja wa Mataifa Dar es salaam, ofisi ya
Waziri Mkuu, UNICEF, UNFPA, UNIC, Ubalozi wa Marekani, Pathfinder, Plan
International na International Youth Foundation.
No comments :
Post a Comment