Tuesday, April 2, 2019

UFUNGUZI WA MAFUNZO KWA WATAALAMU WA HUDUMA YA MIONZI


IMG_20190401_202236_078
NA EMMANUEL MBATILO
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kushirikiana na agency inayoshughulikia maswala ya atomic inayoitwa International atomic energy atomic wamefungua mafunzo kwa wataalamu kujifunza namna ya kuboresha ubora wa hutoaji huduma za mionzi. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika  mganga mkuu wa serikali  Mohammed Kambi amesema kujitokeza kwa wataalamu kutoka katika nchi za Afrika kwenye mafunzo hayo watabadilishana mawazo na kujifunza namna ya kuhakikisha ubora wa huduma zinazotolewa ziko vizuri. 
Aidha kwa upande wa mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Saratani Ocean Road, Julius Mwaisalege amesema kuwa katika mafunzo hayo wanataka kuwajengea uwezo wa kutumia njia bora na sahihi katika mashine zinazotumika katika huduma ya Nuclear medicine.
“Ni muhimu sana utumiaji wa hii dawa (Nuclear medicine) pamoja na uchunguzi wa hizi mashine uweze kutolewa kwa njia sahihi sana kama unavyojua mionzi ni mizuri katika tiba na si salama kama mtu atatumia kwa njia isiyosahihi”. Amesema Mwaisalage.
Mafanzo hayo yatachukua siku tano kuanzia leo Aprili 1 mpaka Aprili 5 ambapo wataalamu kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika wamehudhulia mafunzo hayo

No comments :

Post a Comment