Monday, April 29, 2019

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA WAADHIMISHA MIAKA 55 YA MUUNGANO



Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda  akiwahutubia washiriki wa hafla ya kuadhimisha
miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika katika Hoteli ya Leela Palace jijini New Delhi, India tarehe 26 Aprili 2019. Katika hotuba yake, Balozi Luvanda alieleza kuwa, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa kihistoria na wa kupigiwa mfano duniani kote. Pia alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India ambao umedumu kwa miaka 58.
Mhe. Balozi Luvanda (wa pili kushoto) kwa pamoja na mgeni rasmi Mhe. Shri Sanjiv Arora ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa
India anayeshughulikia Masuala ya Kikonseli, Paspoti, Visa na Diaspora wa (kushoto) na wageni waalikwa wakionesha jarida kuhusu miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuzinduliwa
rasmi katika hafla hiyo.
Mhe. Balozi Luvanda (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mhe. Shri Sanjiv Arora ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Nje wa India anayeshughulikia Masuala ya Kikonseli, Pasipoti, Viza
na Diaspora wa India wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya
Muungano.
Mhe. Balozi Luvanda akiwa
katika picha ya pamoja na Mabalozi wa nchi mbalimbali walioudhuria hafla ya
kuadhimisha miaka 55 ya Muungano.
Mhe. Balozi Luvanda (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania, New Delhi wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano.
 

No comments :

Post a Comment