Mkurugenzi mtendaji wa
bodi TGNP maendeleo, Lilia Liundi akizungumza na wadau mbalimbali
katika mjadala wa bajeti ya mwaka 2019-2020
Wadau mbalimbali wakifuatilia mjadala wa bajeti ya mwaka 2019-2020
…………………….
NA EMMANUEL MBATILO
TGNP Mtandao
kushirikiana na wadau mbalimbali hapa nchini wameandaa mjadala kabla ya
bajeti kuu 2019-2020 la dhumuni la ... kutathimini utekelezaji wa mpango wa
taifa wa pili na hatua iliyofikia nchini katika kutatua usawa wa jinsia
na uwezeshaji wa wanawake.
Akizungumza na
wanahabari jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa bodi TGNP Mtandao, Asseny
Muro amesema mojawapo ya mikakati inayotumiwa na TGNP Mtandao katika
kuleta maendeleo katika jamii hasa usawa wa jinsia na haki za jamii ni
uchambuzi wa sera na mipango na bajeti kwa walengwa wa jinsia.
“Shirika limerasmisha
programu ya uchambuzi wa bajeti kwa baadhi ya almshauri, wizara na
bajeti ya taifa na hii imekuwa ni programu kubwa ya shirika katika
kutengeneza taarifa zitakazoendelea kutumika katika kudai na kuhamasisha
utekelezaji wa sera na bajeti yenye mlengwa wa jinsia”. Amesema Asseny.
Aidha Asseny amesema
kuwa mwaka huu TGNP imeratibu jukwaa la kuwashirikisha wadau mbalimbali
kujadili na kutoa mapendekezo yao yatakayowezesha uboreshaji na
utekelezaji wabajeti ya mwaka 2019 na 2020 kwa mlengwa wa jinsia.
“Kumuwezesha kila
mmoja kutathimini utekelezaji wa maswala ya jinsia kwa kuangalia
mikataba na maadhimio mbalimbali kama vile dira ya maendeleo ya taifa
2025”. Ameongeza Asseny.
Hata hivyo kwa upande
wa mkuu wa idara ya utafiti na uchambuzi wa sera TGNP mtandao, Happiness
Maruchu amesema kuwa lengo kuu la bajeti hiyo ni kuhakikisha linainua
makundi yaliyopo chini kwa kutenga rasirimali za kutosha katika
kushughulikia changamoto zao.
“Tunaona msisitizo
mkubwa wa bajeti tangu mwaka 2016 ipo sana kwenye ujenzi wa miundombinu
na sisi kwa mtazamo wetu si kwamba ujenzi wa miundombinu ni kitu kibaya
hapana tunahitaji kuchochea uchumi kwasababu uchumi ukikuwa
tunatengeneza ajira”. Amesema Happiness.
No comments :
Post a Comment