Tuesday, April 2, 2019

BUNGE LAMKATAA CAG

54237193_2534873866540634_5971838958384125186_n-600x343
 
Na.Alex Sonna,Dodoma
BUNGE la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania limeazimia kwa kauli moja na kutoa hatia kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali(CAG), Profesa Mussa Assad na kukataa kufanya naye kazi na kushirikiana naye katika jambo lolote.
Aidha limetoa  adhabu kwa  Mbunge wa Kawe, Mhe.Halima Mdee kwa  kusimamishwa kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge mpaka bunge la mwezi wa tisa (Septemba) ambapo adhabu yake itamalizika Kamati ya kudumu ya bunge haki, maadili na madaraka ya bunge imetoa taarifa yake kuhusiana na sakata hilo.
 Mwenyekiti wa kamati Emmanuel Mwakasaka,amesoma taarifa hiyo ambapo  amesema kuwa  Kamati imejiridhisha pasina shaka kuwa kauli aliyoitoa CAG Asadi akiwa nchini Marekani akihojiwa na katika kituo cha redio cha idhaa ya kiswahili umoja wa mataifa zililenga kuridharirisha bunge la Tanzania na hivyo kamati imesisitiza haiko tayari kufanya tena kazi na CAG  Asadi.
Mwakasaka amefafanua kuwa,  kwa kitendo cha Profesa Assad kushikilia msimamo wa kauli yake na kukataa kuomba radhi ni dharau kubwa  kwa bunge na taifa kwa ujumla, hivyo wanasitisha kufanya naye kazi wala kushirikiana naye kwa chochote.
Kuhusu azimio la Mdee, amesema alipohojiwa na kamati alikiri kuunga mkono kauli iliyotolewa na Profesa asadi licha ya kuwa yeye hakulenga kulidhalilisha bunge wala kudharau muhimili huo.
Amesema hata hivyo mdee hakuonyesha kujutia kauli yake ya kuunga mkono na wala hakuomba radhi mbele ya kamati.
Hata hivyo Mwenyekiti amesema kuwa hiyo ni mara ya nne  kwa Mbunge huyo kuitwa mbele ya kamati hiyo kuhojiwa  makosa mbalimbali ikiwemo kudharau kiti cha Spika na mara zote tatu alipewa adhabu.
Amesema Januari 2019 baada ya kamati kumhoji walijiridhisha ana hatia na kuazimia kumpa adhabu ya kutohudhuria vikao viwili vya Bunge kwa maana ya kikao chote cha Bunge hili la bajeti kinachoendelea na kikao cha Septemba mwaka huu.

No comments :

Post a Comment