Na Ahmed Mahmoud Longido
Mawaziri wa Kenya na
Tanzania wamekutana kutatua changamoto za mipakani Kati ya nchi hizo
mbili ili kuongeza ufanisi na kuondoa changamoto Kwa Wafanyabiashara wa
pande hizo mbili.
Mawaziri wa Biashara
kutoka nchi za Kenya na Tanzania wamekutana kujadili na kutatua
changamoto za kibiashara katika mipaka ya nchi hizo ikiwa ni pamoja na
kuskiliza kero za wafanyabiashara na kuzipatia ufumbuzi ili kuondokana
na usumbufu wanaoupata wafanyabiashara.
Wafanyabiashara hao
wameeleza changamoto ya mizigo yao kukaa muda mrefu mipakani humo pamoja
na changamoto ya hati za muda za kusafiria madereva kutolewa kwa muda
mfupi hivyo kuathiri biashara hivyo wameomba hati hizo zitolewe kwa muda
wa mwaka mmoja na si kwa safari moja pekee
Waziri wa biashara
nchini Kenya Chris Kibito amesema kuwa asilimia 45% ya biashara ya
afrika mashariki inafanyika kati ya Tanzania na Kenya hivyo ni vyema
kuimarisha mahusiano ya kibiashara ili nchi zote mbili ziweze kunufaika
pia ameahidi kushughulikia kwa karibu changamoto wanazokutana nazo
wafanyabiashara mipakani humo
Amesema kuwa mbali na
biashara kuchelewa mipakani kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo
suala zima la upimaji wa viwango vya bidhaa zinazovuka watajitahidi
kuhakikisha masuala yote yanatatuliwa ndani ya miezi mitatu.
Amesema malengo ya
biashara ni kukuza uchumi Kwa upande mmoja na hivyo kama suala hilo
halikuchukuliwa Kwa kuliangalia Kwa ndani kuondoa changamoto basi
hatutapiga hatua kiuchumi.
Waziri wa biashara na
viwanda nchini Tanzania JOSEPH KAKUNDA amesema kuwa changamoto
zilizofikishwa na wafanya biashara hao wanazifanyia kazi kwa kushrikiana
na maslahi mapana ya nchi zote hivyo kuwaomba wafanyabiashara hao kuwa
na uvumilivu wakati wakisubiri majibu ya changamoto hizo.
Amesema kuwa hakuna
nchi hata moja ambayo inataka kuona changamoto za kibiashara kwenye
mipaka hivyo ndio maana wamekutana kujadili na kuona namna nzuri ya
kuondoa changamoto za kibiashara mipakani mwa nchi hizo
Mawaziri kutoka nchi
za Kenya na Tanzania wameweka saini ya makubaliano ya kukutana mara
mbili kwa mwaka ili kutatua changamoto za kibiashara na kuimarisha
mahusiano.
No comments :
Post a Comment