Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma
Sosteneth Kibwengo akizungumza na wanahabari hawapo pichani, akitoa
taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa robo ya mwaka.
……………………………
Na EZEKIEL MTONYOLE, DODOMA.
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na
rushwa TAKUKURU, Mkoa wa Dodoma, imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi
milioni mia moja hamsini na mbili zilizokuwa zilipwe kwa
wakandarasi
ambao hawakutimiza majukumu yao kikamilifu katika miradi waliyopewa.
Pia jumla ya shilingi milioni
mia tisa(9000,000,000) zinachunguzwa baada ya kuwa na viashiria vya
rushwa katika miradi mbalimbali.
Hayo yamebainishwa leo mkoani
hapa na kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU,
mkoa wa Dodoma Sosteth kibwengo wakati akitoa taarifa ya robo ya mwaka
kwa wanahabari.
Ambapo amesema kwa robo ya
mwaka taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi mia moja na
hamsini na mbili(152), zilizokuwa zilipwe kwa wakandarasi ambao
hawakutekeleza majukumu yao kikamilifu.
“Katika miradi iliyofuatiliwa,
fedha Sh. milioni mia tisa (900,000,000) inachunguzwa baada ya
viashiria vya jinai kuonekana, TAKUKURU pia imefanikiwa kuokoa kiasi cha
Sh. milioni mia moja hamsini na mbili na laki tatu (152,300,000) ambazo
zingelipwa kwa wakandarasi ambao ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi ya
maji umebaini hawakutimiza majukumu yao ipasavyo” amesema Kibwengo.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa pia imemtaka mkurugenzi wa kampuni ya Global Space East Africa
Limited, inayojenga kituo cha afya Mima kilichopo Wilayani Mpwapwa
mkoani hapa kulipoti katika ofisi ya zake zilizopo wilayani humo kwa
mahojiano.
“Pia tumebaini udanganyifu katika
mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Mima wilayani Mpwapwa hivyo
tunamtaka Mkurugenzi wa kampuni ya Global Space East Africa Limited ya
Dare esaalam, bw. Gaston Meltus Francis ambaye kampuni yake ilipewa kazi
hiyo kuripoti mara moja kwenye ofisi zetu za wilaya ya Mpwapwa”
amesema.
Vile vile alibainisha kuwa
katika kipindi husika, TAKUKURU ilipokea jumla ya taarifa tisini na sita
(96) za rushwa na makosa yahusianayo ambapo sekta ziliongoza kwa
tuhuma mi.
Serikali za mitaa (25%), Ardhi
(17%), Elimu (16%), Afya (8%), Maji, Ujenzi na Mahakama (kila moja
asilimia 7), na Polisi (6%), taarifa hizo zilifanyiwa kazi kwa njia
mbalimbali na majalada nane (8) ya uchunguzi yalikamilika ikiwa ni
ongezeko la asilimia 12.5 ya majalada yaliyokamilika kwa kipindi hicho
mwaka 2018.
Aidha tumefungua kesi mpya
tano (5) na kesi nne (4) zilitolewa maamuzi na Mahakama ambapo Jamhuri
imeshinda zote kwa washtakiwa kutiwa hatiani na kuhukumiwa vifungo
mbalimbali.
Aidha alisema kwa robo ya
Aprili hadi Juni, 2019, pamoja na majukumu mengine TAKUKURU inakusudia
kuongeza juhudi katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati
mkoani Dodoma ikiwemo ya ujenzi wa barabara; kuchambua mifumo ya
ukusanyaji wa kodi na mapato ya serikali; na kuendelea kuelimisha umma
madhara ya rushwa katika uchaguzi.
Vile vile alibainisha kuwa
TAKUKURU inawataka wajumbe wa Kamati za Ujenzi na Manunuzi wa miradi
mbalimbali ya maendeleo kuzingatia taratibu za matumizi ya fedha za
serikali na kuwaasa wasikubali kurubuniwa na viongozi wasio waadilifu
kwani wao ndio watakaowajibika.
Pia aliwataka watendaji kutoa
nyaraka tunazohitaji kisheria kwa wakati ili waweze kutekeleza majukumu
yao na kuwaasa wale wanaojaribu kukwamisha kwamba kitendo hicho ni kosa
la jinai na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.
No comments :
Post a Comment