Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa
akizungumza na washiriki waliohudhuria katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya
Shirika la Compassion International Tanzania yaliyofanyika Aprili 27,
2019 katika ukumbi wa Kanisa la TAG lililopo Kata ya Miyuji, Jijini
Dodoma.
Mkurugenzi wa Taifa wa Shirika la
Compassion International Tanzania, Bi. Agness Stanley Hotay akielezea
kuhusu huduma zinazotolewa na Shirika la Compassion International
Tanzania wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa
(wa pili kutoka kushoto) akifuatilia nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na
wanakwaya ya Muunganiko wa Makanisa ya Kiinjili wakati wa hafla hiyo
iliyofanyika Jijini Dodoma ikiwa ni Maadhimisho ya Miaka 20 ya Shirika
la Compassion International Tanzania.
Afisa Maendeleo ya Vijana, kutoka
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Happy
Mwaipopo akielezea jambo kuhusu Mikopo inayotolewa na Ofisi hiyo kupitia
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Baadhi ya Maaskofu kutoka kwenye
Makanisa ya Kiinjili hapa nchini wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe.
Stella Ikupa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa hafla
hiyo.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu
wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza
wakati wa hafla hiyo.
Sehemu ya Washiriki wa
walioudhuria kwenye hafla ya Maadhimisho ya Miaka 20 ya Shirika la
Compassion International Tanzania yaliyofanyika Jijini Dodoma, Aprili
27, 2019.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa
akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taifa wa Shirika la Compassion
International Tanzania, Bi. Agness Stanley Hotay.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa
akipongezwa na Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhe. Lolensia Bukwimba (Kulia)
mara baada kusoma hotuba yake.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa
akisikiliza kwa mmoja wa vijana wanaohudumiwa na Shirika la Compassion
International Tanzania namna wanavyotengeneza bidhaa za Viatu vya ngozi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa
(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na waratibu wa Shirika la
Compassion International Tanzania na watendaji wa Ofisi yake. Wa pili
kutoka kulia ni Mbunge wa
Jimbo la Busanda Mhe. Lolensia Bukwimba, (wa
tatu kutoka kushoto) ni Mkurugenzi wa Taifa wa Shirika la Compassion
International Tanzania, Bi. Agness Stanley Hotay.
………………………………………………………………………………………..
Na. Mwandishi Wetu
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa
amelipongeza Shirika lisilo la kiserikali la Compassion International
Tanzania (CIT) kwa kuwahudumia na kuwapatia watoto na vijana stadi za
maisha zinazowawezesha kujitegemea.
Naibu Waziri Ikupa ametoa pongezi
hizo wakati wa Maadhimisho ya Miaka 20 ya Shirika hilo yaliyofanyika
leo Aprili 27, 2019 katika ukumbi wa Kanisa la TAG lililopo Mipango,
Jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yalikuwa na Kauli Mbiu isemayo; “Wekeza
kwa Watoto na Vijana kwa Uchumi Endelevu.”
Alieleza kuwa Shirika la
Compassion International Tanzania limekuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha watoto na vijana nchini wanahudumiwa na kuondokana na hali
ya umasikini kwa kuwa chachu ya maendeleo kwa jamii na Taifa.
“Shirika hili ni la mfano na
limeendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwalinda watoto na
kuwapa fursa ya kufikia ndoto zao na kuwapatia vijana ujuzi wa stadi za
maisha zinazoleta mabadiliko chanya kwao na kuwaletea maendeleo yao
binafsi na Taifa kwa ujumla,” alisema Ikupa
Aliongeza kuwa Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekuwa
akionesha watanzania namna gani nchi yetu imeweza kujitegemea katika
kutekeleza shughuli mbalimbali, hivyo Mhe. Rais ni mfano tosha wa kuigwa
na vijana nchini kwa kuona wanauwezo wa kujitegemea.
Aidha, Naibu Waziri Ikupa alitoa
rai kwa vijana kuacha kukaa kwenye vijiwe bila sababu za msingi na
kubadili mitazamo, bali watumie muda wao kutafakari shughuli za kufanya
kwa bidii ambazo zitawaletea maendeleo na kuwawezesha kujikwamua
kiuchumi.
“Serikali imekuwa ikitoa mikopo
kwa vijana ili waweze kuanzisha shughuli mbalimbali zitakazo wawezesha
kukua kiuchumi, tumieni fursa ya ujuzi mliopata kupitia shirika hili na
ubunifu mlionao kuchangamkia fursa hiyo muhimu itakayowawezesha
kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo viwanda,” alisema Ikupa
Pia alitoa wito kwa jamii
kuripoti haraka vitendo vya unyanyasaji wa watoto katika madawati ya
jinsia na watoto yaliyopo kwenye vituo vya polisi nchini na kwa maafisa
ustawi wa jamii ili kutokomeza vitendo hivyo kwa kumjengea mazingira
salama motto na kumuonesha jamii yake imejaa upendo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Taifa wa Shirika la Compassion International Tanzania, Bi. Agness
Stanley Hotay alisema kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika
kuhakikisha wanawatetea na kuwasimamia watoto na kuwapatia nafasi vijana
ya kujitambua kwa kuchangamkia fursa ambazo zipo katika jamii na kuleta
ufumbuzi wa kimaendeleo.
“Maono ya shirika ni kuona
wanufaika wanatoka katika uhitaji na kujijengea dhana ya kujitegemea,
vilevile kuwa wahisani wa watu wengine,” alisema Hotay
Shirika la Compassion
International Tanzania (CIT) ni sehemu ya Compassion International
ambalo ni shirika la kimataifa la Kikristo linalojihusisha kuhudumia
watoto na vijana wanaotoka katika kaya maskini kwa njia ya ufadhili.
Shirika hili limekuwa likifanya huduma hii hapa nchini toka mwaka 1999.
Kwa sasa Shirika hilo lipo katika
Mikoa 19 ya Tanzania Bara ambayo ni Arusha, Dar es Salaam, Kigoma,
Manyara, Pwani, Morogoro, Iringa, Dodoma, Kilimanjaro, Singida,
Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Lindi, Geita, Mtwara, Simiyu na Kagera.
No comments :
Post a Comment