Sunday, April 28, 2019

Hakuna Chama cha Siasa kitakachozuia Ushindi wa CCM 2020

????????????????????????????????????
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Leila burhan Ngozi akizungumza na Vijana mbali mbali katika Tawi la CCM Miti Ulaya lililopo Jimbo la Malindi.
????????????????????????????????????
VIJANA wa UVCCM wakiwa katika matembezi ya Amsha amsha ya kuimarisha Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Malindi Zanzibar wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Leila burhan Ngozi.
????????????????????????????????????
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Leila burhan Ngozi akikabidhi Cheti kwa mshiriki wa Matembezi ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa mwaka 2019.
…………………………………………………………………………………..
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Leila Burhan Ngozi amesema hakuna Chama cha Siasa chochote kitakachozuia Ushindi wa CCM kwa ngazi zote
katika Jimbo la Malindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Msimamo huo ameutoa leo katika Matembezi ya kuimarisha uhai wa Chama ya ‘Amsha amsha’ yenye kauli mbiu ya Malindi ya Kijani inawezekana ya kushusha Bendera kongwe na kupandisha mpya katika Matawi,Maskani ,Ofisini na Majengo mbali mbali yanayomilikiwa na CCM na Jumuiya zake katika Jimbo hilo.
Alisema mwaka 2020 ndio wakati mwafaka wa kulikomboa Jimbo hilo likarudi mikononi mwa CCM hatua itakayopelekea Wananchi wa eneo hilo kuendelea kunufaika na Matunda ya Serikali za Chama Cha Mapinduzi.
Alisema CCM ina nafasi ya Mwakilishi na Madiwani na Mbunge ni wa upinzani hali inayopelekea kutokuwepo kwa ushirikiano katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwani wapinzani wamekuwa wakikwamisha kwa makudi mipango ya maendeleo huku CCM ikitoa Huduma kwa Jamii kupitia Mwakilishi wake.  
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu Leila, alifafanua kwamba ridhaa ya kulitwaa Jimbo hilo kuwa la CCM itatoka kwa Wananchi wenyewe ambao wameonyesha nia ya kuiamini CCM.
Katika maelezo yake Leila, alieleza kwamba CCM tayari inajivunia Utekelezaji mzuri wa Ilani yake katika maeneo mbali mbali Nchini likiwemo Jimbo la Malindi, hatua inayotakiwa kupongezwa na kila mwananchi ambaye ni Mzalendo.
Alisema kasi ya CCM ya kuwapelekea wananchi maendeleo endelevu itaendelea kuongezeka kila siku zikienda kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, kwani Wananchi wanataka maendeleo na sio maneno ya porojo na ahadi hewa.
Alizisisitiza Jumuiya zote za Chama Cha Mapinduzi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa mujibu wa kanuni na miongozo yao ili mwaka 2020 CCM ishinde kwa kishindo.
Pamoja na hayo aliupongeza Uongozi wa UVCCM Wilaya ya Mjini kwa kuanzisha kampeni hiyo ya ‘Amsha amsha’ katika Jimbo la Malindi inayoimarisha uhai wa Chama  na Jumuiya zake kwa ujumla.
Alisema changamoto zote zilizotajwa katika risala za Matawi ya Vijana zinazotakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa haraka ataziwasilisha katika ngazi za Uongozi wa CCM ili zitafutiwe ufumbuzi wa kudumu.
Aliwakumbusha Vijana kuchangamkia fursa za Kielimu zilizopo nchini sambamba na kujiunga na Vituo mbali mbali vya Mafunzo ya Amali ili wapate ujuzi na utaalamu wa kuwawezesha kujiajili wenyewe.
“Serikali zetu zipo katika Safari ya kutafsiri kwa vitendo Sera ya Uchumi wa Viwanda kwa kuaulisha Viwanda Vidogo Vidogo na Vikubwa vifanye kazi ili wananchi wapate ajira lakini pia tuzalishe bidhaa nyingi na kuuza nje ya Nchi kwa lengo la kuingiza fedha za Kigeni.”,alisema Leila.
Aliwasihi Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha wanaongeza wanachama wapya watakaopiga kura za ndio zitakazokipatia ushindi Chma mwaka 2020 na kiendelee kuongoza Dola.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Kamaria Suleiman Nassor alisema matembezi hayo katika Jimbo hilo wanajaribu mitambo ya kuelekea katika uringo wa Mapambano ya Kisiasa ya mwaka 2020.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mjini Hudhaima Mbarouk Tahir, aliwashukru Vijana mbali mbali wa UVCCM walioshiriki katika amsha amsha hiyo iliyohamasisha Wanachama wa CCM na kutuma ujumbe mzito kwa wapinzani wa Jimbo la Malindi.
Hudhaima alieleza kuwa matembezi hayo yatakuwa endelevu katika Majimbo mbali mbali yaliyopo katika Wilaya hiyo kwani ni sehemu ya kuwaunganisha Vijana na kuwajenga kuwa wazalendo wa kukipenda Chama Cha Mapinduzi muda wote.
Kupitia matembezi hayo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Leila Burhan Ngozi amewatunuku Vyeti Vijana mbali mbali walioshiriki matembezi ya kuwaenzi Waasisi wa Mapinduzi ya mwaka 2019,ametoa Kadi za Uanachama kwa Wanachama wapya wa UVCCM pamoja na kupandisha Bendera katika Ofisi za Chama na Jumuiya pamoja na kutembelea kikundi cha Ushirika.

No comments :

Post a Comment