Wednesday, April 3, 2019

MWALIMU ALIYE OWA WANAFUNZI 10 DARASA LA KWANZA ASHITAKIWA BUNGENI


Bunge-1
Na Alex Sonna,Dodoma
BUNGE limeelezwa kuwa mkoani Mara kuna mwalimu ambaye amewafanya kama wake zake watoto 10 wa darasa la kwanza.
Mbunge wa Malindi, Ally Salehe (CUF), alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali bungeni
ambapo amedai kwamba kuna tatizo la ubakaji limezidi kuwa kubwa nchini.
Amefafanua kuwa tatizo la ubakaji wa watoto linaonekana ni kubwa hapa nchini, tume ya Katiba na sheria hivi karibuni walienda Mara na wakapata taarifa za kutosha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima kuhusiana na mwalimu huyo.
“Kuna mwalimu amewafanya wake zake watoto 10 wa darasa kwanza na kuna taarifa nyingi za vitisho juu ya ubakaji kwa watu wazima na watoto,”amesema.
Mbunge huyo akataka kujua kama Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee pamoja na Bunge haioni haja ya kuunda Tume ya kutafuta utaratibu wa kwenda kulishughulikia jambo hili.
Amesema tatizo ni kubwa na ukubwa wake unafikia mpaka watu wanauliwa na wengine wanakimbilia upande wapili wa Kenya, Serikali ifikirie juu ya jambo hilo kwa undani.
Baada ya swali hilo, Spika wa Bunge, Jon Ndugai akachombeza kwa kumwambia Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko kwamba sio wanaongoza kwa mambo mengine tu kumbe na hayo.
Akijibu swali hilo,kwa niaba, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dk.Harisson Mwakyembe amesema jambo hilo ni baya na linatakiwa litafutiwe ufumbuzi.
“Moja ya shinikizo kubwa katika Nchi za Magharibi ni shinikizo la ndoa za jinsia moja shinikizo la ushoga kama haki za kibinadamu….
“Bado Nchi 38 kati ya 54 za Afrika zinapinga mambo hayo na Tanzania ikiwepo yaani vitendo hivyo ni vya jinai na mtu anafungwa,”amesema.
Mwakyembe ameeleza kuwa changamoto katika jamii ni ndugu  kuwaficha mashahidi hali ambayo imekuwa ikiwapa wakati mgumu.
“Tatizo kubwa ni kwamba jamii inaficha haya matatizo mfano matatizo ya watoto kulawitiwa yanafanyika sehemu kubwa na ndugu katika jamii na tukianza upelelezi familia zina walinda wale wanaotakiwa kutoa ushahidi. 
Amesema katika sheria kama hakuna ushahidi huwezi ukamfunga mtu kwahiyo sasa hivi ni kosa kubwa na adhabu ni kali.
Ametoa wito kwa watanzania kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili tuweze kuwapa hao wahalifu wanaojaribu kuchafua kizazi cha kesho.

No comments :

Post a Comment