Wednesday, April 3, 2019

DKT.MAHIGA AHIMIZA MAELEWANO NA MAHUSIANO MAZURI KWA WATUMISHI WA WIZARA YAKE


AA
WAZIRI WA Katiba na Sheria Dkt. Augustine Mahiga akiwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju na wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa kuanza kwa kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika jijini Arusha,
IMG_4110A
Wajumbe wa kikao cha baraza la Wafanyakazi Wizara ya Katiba na Sheria wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa kuanza kwa kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika jijini Arusha,
IMG_4113A
Wajumbe wa kikao cha baraza la Wafanyakazi Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria hayupo pichani alipokuwa akizungumza nao katika  kikao cha Baraza la Wafanyakazi Wizara hiyo kilichofanyika jijini Arusha,
IMG_4116A
Wajumbe wa kikao cha baraza la Wafanyakazi Wizara ya Katiba na Sheria wakiendelea na  kikao cha Baraza la Wafanyakazi Wizara hiyo kilichofanyika jijini Arusha,
IMG_4118A
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Bw. Blastus Kahemela aliesimama akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi Wizara hiyo kilichofanyika jijini Arusha,
IMG_4121A
wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mahiga jijini Arusha wakati wa kikao cha Baraza hilo lililofanyika Aprili 3, 2019 
……………
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amewaambia watumishi wa Wizara kuwa
tija na ufanisi vitapatikana iwapo kutakuwa na maelewano na mahusiano mazuri kati ya uongozi wa Wizara na watumishi.
Mhe. Dkt. Mahiga alipokuwa akizungumza na Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Katiba na Sheria lililokutana jijini Arusha kujadili masuala mbalimbali ya wizara hiyo.
Aidha Dkt Mahiga amewapongeza watumishi hao na viongozi wao kwa kukamilisha ujenzi wa jingo jipya la Wizara lililoko katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.    
“Nichukue nafasi hii kuwapongeza kwa kazi nzuri mlioifanya ya kukamilisha ujenzi wa ofisi mpya ya Wizara kwa haraka na ufanisi mkubwa, hiki ni kitu cha kujivunia na binafsi nawapongeza sana,” alisema Dkt. Mahiga.
Baraza la Wafanyakazi la Wizara limekutana katika kikao chake cha kawaida ambacho kilipitia hija mbalimbali ambazo uongozi wa Wizara ulizitolea maelezo juu ya namna utekelezaji wake ulivyofanyika na hivyo kuleta tija na ufanisi katika utendaji kazi wa wizara.
Baraza hili limefanyika chini ya Mwenyekiti wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome, Katibu wake Bw. Blastus Kahemela na kuhudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju, wajumbe wa menejimenti ya Wizara na watumishi wa Wizara ambao ni wawakilishi wa watumishi wengine wa Wizara.

No comments :

Post a Comment