Saturday, April 27, 2019

MATUKIO KATIKA PICHA: WAZIRI MKUU MAJALIWA, SPIKA NDUGAI WASHUHUDIA MECHI TIMU YA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR JIJINI DODOMA


V25A3244AA
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akipokelewa na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyochezwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mwenye Kijani ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mbunge Viti Maalum, Mhe. Salma Kikwete (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Pastobas Katambi (katikati). Mechi hiyo iliisha kwa timu zote mbili kufunga magoli 2 -2, Lengo likiwa ni kuboresha uhusiano baina ya Mabunge hayo
V25A3219AA
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiteta jambo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu kati ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyochezwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mechi hiyo iliisha kwa timu zote mbili kufunga magoli 2 -2, Lengo likiwa ni kuboresha uhusiano baina ya Mabunge hayo
V25A3364AA
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia), Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) wakifuatilia mechi kati ya timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyochezwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Watatu kushoto ni Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Pastobas Katambi
V25A3413AA
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakishangilia goli walilofunga dhidi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar mchezo uliochezwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Mch. Peter Msigwa, Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi na Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto ambaye pia ni mfungaji wa goli hilo na nyuma ni Ndg. Onesmo lau lau. Katika mchezo huo timu hizo zilifungana magoli 2 -2, Lengo likiwa ni kuboresha uhusiano baina ya Mabunge hayo
V25A3323AA
Wachezaji wa timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kulia) wakisalimiana na Wachezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki baina yao iliyochezwa katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mechi hiyo iliisha kwa timu hizo kufungana magoli 2 -2, Lengo likiwa ni kuboresha uhusiano baina ya Mabunge hayo
V25A3393AA
Mbunge wa Kilolo, Mhe. Venance Mwamoto (katikati) ambae pia ni Kocha Mchezaji na Mfungaji wa bao la kwanza la timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Wachezaji wa timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mapumziko katika mechi iliyowakutanisha timu hiyo na timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mechi hiyo iliisha kwa timu hizo kufungana magoli 2 -2, Lengo likiwa ni kuboresha uhusiano baina ya Mabunge hayo
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

No comments :

Post a Comment