Katibu Tawala Mkoa wa kagera
Profesa Faustin Kamuzora akizungumza wakati wa mkutano wa mahusiano
kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda
unaofanyika Bukoba mkoani Kagera, wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe,
kushoto ni Balozi Paul Mkumbya kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda
na kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Paul Makelele.
Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki
Mkutano wa Mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania
na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera wakimsikiliza Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja
Mnyepe (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa
mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda
unaofanyika Bukoba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika (kulia) akisisitiza jambo kwa
wajumbe wa Tanzania wanaoshiriki mkutano wa mahusiano kujadili
changamoto zinazoikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba
mkoani Kagera. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo Elisante
Ole Gabriel na anayemfuatia ni Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe.
Balozi wa Tanzania nchini Uganda
Dkt Aziz Mlima (Kushoto) akimsikiliza Mpima Mkuu wa Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Julius Msofe (wa pili kulia) wakati wa
mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania
na Uganda unaofanyika Bukoba mkoa wa Kagera. Kulia ni Mthamini Mkuu wa
Serikali Evelyne Mugasha.
Balozi wa Tanzania nchini Uganda
Dkt Aziz Mlima (wa tatu Kulia) akizungumza wakati wa kujadiliana na
ujumbe wa Uganda katika mkutano wa mahusiano kujadili changamoto
zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani
Kagera. Kulia ni Mthamni Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha. (PICHA NA
WIZARA YA ARDHI)
……………………..
Na Munir Shemweta, WANMM BUKOBA
Makatibu Wakuu wa Tanzania na
Uganda wanakutana mjini Bukoba mkoani Kagera katika mkutano wa mahusiano
kujadili changamoto zinazozikabili nchi hizo ikiwemo Uimarishaji Mpaka
wa Kimataifa pamoja na Matumizi endelevu ya rasilimali za Bonde la mto
Kagera..
Mkutano huo wa siku mbili umeanza
tarehe 29 April 2019 mjini Bukoba na kuwakutanisha
Makatibu Wakuu wa
nchi hizo mbili kutoka Wizara za Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mifugo,
Wizara ya Maji pamoja na Wizara ya Nishati.
Kabla ya mkutano huo, Wataalamu wa
sekta shiriki kutoka Tanzania na Uganda walikutana na kujadiliana
kuhusiana na changamoto zinazozikabili nchi hizo mbili kwa nia ya
kuwasilisha mapendekezo yaliyofikiwa kwa Makatibu Wakuu wa nchi hizo.
Baadhi ya Changamoto
zinazojadiliwa kwenye mkutano huo, ni pamoja na Uimarishaji na Uthamini
wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Uganda, Mpango kabambe wa utunzaji
mto Kagera na Matumizi endelevu ya rasilimali kati ya Tanzania na
Uganda katika Bonde la Mto Kagera.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe alisema mkutano huo ni
mfululizo wa mikutano kati ya nchi hizo mbili wenye lengo la kutatua
changamoto zinazozikabili nchi hizo kwa nia ya kuleta maendeleo.
Alisema, pamoja na kuwepo
changamoto kadhaa lakini Tanzania na Uganda zinaendelea kufurahia
mahusiano mazuri yaliyopo kwa kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali
yenye lengo la kuleta manufaa kwa nchi na watu wake.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa
wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora aliuzungumzia mkutano huo kama njia
ya kuzifanya nchi husika kufanya kazi pamoja na kuzidisha ushirikiano
wenye nia ya kuleta maendeleo na kusisitiza kuwa, utekelezaji wa
makubaliano yatakayofikiwa unapaswa kufanywa kwa wakati.
No comments :
Post a Comment