Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola akiingia Kituo cha Polisi Stakishari, jijini Dar es Salaam
alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo hicho kwa lengo la kuboresha
utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini. Pia Lugola aliwahoji wananchi
waliofika kuwachukulia dhamana ndugu zao waliopo ndani ya kituo hicho,
pamoja na mahabusu wote waliopo kituoni hapo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola (kulia), akiwahoji wananchi mbalimbali katika mapokezi ya
Kituo cha Polisi cha Stakishari, jijini Dar es Salaam, leo, walipofika
kituoni hapo kwa ajili ya kuwachukulia dhamana pamoja na kupata huduma
zinginezo kituoni hapo. Pia Lugola aliwahoji wananchi waliofika
kuwachukulia dhamana ndugu zao waliopo ndani ya kituo hicho, pamoja na
kuwahoji mahabusu wote waliopo kituoni hapo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya
Kipolisi Ukonga, jijini Dar es Salaam, Frank Duma, alipokua anatoa
taarifa ya utendaji kazi ya Wilaya hiyo. Waziri huyo alifanya ziara ya
kushtukiza katika Kituo cha Polisi cha Stakishari yenye lengo la
kufuatilia utendaji kazi katika kituoni hapo. Pia Lugola aliwahoji
wananchi waliofika kuwachukulia dhamana ndugu zao waliopo ndani ya kituo
hicho, pamoja na kuwahoji mahabusu wote waliopo kituoni hapo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola akiongozana na viongozi wa Kituo cha Polisi cha Stakishari,
jijini Dar es Salaam, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza
katika kituo hicho, leo. Lugola aliwahoji wananchi waliofika
kuwachukulia dhamana ndugu zao waliopo ndani ya kituo hicho, pamoja na
mahabusu wote waliopo kituoni hapo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
…………………..
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Kangi Lugola, amefanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Polisi
Stakishari jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia utendaji kazi wa
Kituo hicho.
Waziri Lugola aliwasili
kituoni hapo Saa 6:16 mchana ambapo alikutana na
wananchi mapokezi ya
kituo hicho ambao walifika kwa ajili ya kuwachukulia dhamana ndugu zao
walipo katika mahabusu ya kituo hicho, aliwahoji kama wanapata huduma
nzuri kutoka kwa askari wa kituo hicho.
Pia Waziri Lugola akiwa katika
mapokezi ya kituo hicho, alikichukua kitabu cha taarifa za watuhumiwa
wote waliopo mahabusu na baadaye kuelekea katika mahabusu hiyo akiwahoji
watuhumiwa wote kwa kuwaita kwa majina kujua makosa yao yaliyoyafanya
wawepo kituoni hapo.
Akizungumza mara baada ya
kumaliza kuiwahoji mahabusu hao, alisema ziara yake ni ya kawaida ya
kufuatilia utendaji kazi wa vituo vya polisi, pia kufuatilia ahadi zake
ambazo alizitoa Bungeni kufuatilia vituo mbalimbali vinavyolalamikiwa,
na pia yeye Waziri ni wajibu wake kufuatilia utendaji kazi pamoja na
maagizo anayoyatoa mara kwa mara ya dhamana zitolewe saa 24 ikiwemo
Jumamosi na Jumapili na pamoja na polisi kutowabambikizia kesi wananchi.
“Lengo la hii ziara yangu ni
kuboresha utendaji kazi wa vituo vya polisi nchini, sijaja kumuadhibu
mtu mimi, hivyo msiwe na wasiwasi, bali kilichonifanya hapa nije
nikufuatilia maagizo mbalimbali ambayo niliyatoa kama kweli mnayafanyia
kazi,” alisema Lugola.
Lugola aliwataka Makamanda wa
polisi mikoa mbalimbali nchini, kusimamia utendaji kazi bora na
kuakikisha maagizo yake anayoyatoa yanafanyiwa kazi ipasavyo, na
ataendelea kuyafuatilia maagizo yote anayoyatoa na endapo yakipuuzwa
hatamvumilia mtu.
No comments :
Post a Comment