Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akisalimia na baadhi ya viongozi wa wilaya ya mkoa wa Dodoma alipowasili
kwa ajili ya kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka
mmoja na nusu katika hospitali hiyo iliyopo Makole jijini Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu,akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kugawa
vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika
hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Mkoa na ambaye ni mratibu wa Malaria mkoa wa Dodoma,
Francis Bujiku,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma
Sehemu
ya akina mama wajawazito wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (hayupo
pichani) wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya
mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini
Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akionesha nchandarua kwa akina mama wajawazito (hawapo pichani) wakati
wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na
nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akiwapongeza baadhi ya wanaume ambao waliwaleta watoto klinik wakati wa
kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu
katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akigawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu
katika hospitali ya Wilaya ya Makole jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangwe blog
…………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu,amesema kuwa Serikali imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa
Malaria kwa asilimia 50 kutoka asilimia 14 mwaka 2015 hadi kufikia
asilimia 7.
Hayo
ameyasema leo wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto
chini ya mwaka
mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya ya Dodoma.
Aidha,amesema
kuwa halmashauri kutenga fedha za ndani kwa ajili ya kununua viuwadudu
ikiwa ni katika kupambana na maambukizi ya Malaria katika maeneo yao.
Waziri
Ummy amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 2 ya utawala wa Rais John
Magufuli, Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya Malaria kwa asilimia
50 kutoka wastani wa asilimia 14 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 7.
Hata hivyo amesema kuwa serikali imekuwa na mikakati mingi ya
kupambana na maambukizi wa ugonjwawa malaria ambayo yamekuwa ikiuwa
Watanzania wengi kuwa mbali na kugawa vyandarua pia wanapulizia dawa
katika mikoa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi.
”Serikali
imenunua takribani lita 60,000 ya viuawadudu kwa ajili ya kuua mazalia
ya mbu na kuzigawa katika mikoa yenye maambukizi makubwa ya malaria kama
vile Mkoa wa Kagera, Geita, Kigoma, Lindi na Mtwara lakini pia niwaombe
wananchi kutunza mazingira ili kujiepusha na mbu waenezao malaria,”
amesisitiza Mwalimu
Aidha,
Mwalimu alisema mkakati wa serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka
2020 angalau wajawazito 80 kati ya 100 waweze kuhudhuria kiliniki
angalau mara nne hivyo kutoa fursa ya kufanyiwa vipimo mbalimbali
ikiwamo malaria.
Kwa
upande wake mratibu wa ugonjwa wa malaria mkoa wa Dodoma, Fransis
Bujiku amesema kuwa Mkoa huo umefanikiwa kupunguza kiwango cha
maambukizi ya malaria kutoka asilimia 1 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia
0.6 kwa sasa.
Bujiku amesema kuwa kwa pamoja wamefanikiwa kwa kutuna mazingira ikiwa ni pamoja na kunyunyiza dawa ya kuua mbu kipindi cha masika na kufukia madimbwi yote yanayotuamisha maji pamoja na kuwahamasisha wananchi kulala kwenye vyandarua.
Bujiku amesema kuwa kwa pamoja wamefanikiwa kwa kutuna mazingira ikiwa ni pamoja na kunyunyiza dawa ya kuua mbu kipindi cha masika na kufukia madimbwi yote yanayotuamisha maji pamoja na kuwahamasisha wananchi kulala kwenye vyandarua.
Siku ya malaria duniani inafanyika kesho ambapo kitaifa itafanyikia
mkoani Lindi ikiwa na kauli mbiu isemayo Ziro malaria inaanza na mimi
No comments :
Post a Comment