Friday, April 26, 2019

MAADILI NDIO UTIMILIFU WA MALENGO KWA WASOMI JUKUMU KAZINI


AA
Na. Majid Abdulkarim
Wanafunzi wa Elimu ya Juu wametakiwa kuwa na maadili mema katika kufikia malengo yao ili kupata elimu bora itakayo wasaidia kazini katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu kipindi watakapo kuwa wamehitimu masomo yao.
Wito huo umetolewa na Kaimu Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro (MUM) Dkt. Yahya Abdallah Tego wakati wa kikao na wanafunzi wa chuo hicho katika
Ukumbi Mkubwa wa Mikutano MUM leo Mkoani Morogoro.
Dtk. Tego amesema kuwa elimu bila maadili hakuwezi kupatikana utendaji utakao leta matokeo bora katika kutekeleza majukumu pale mtakapo kuwa mmehitimu masomo yenu.
Aidha Dtk.Tego amewataka wahadhili wa chuo hicho kusimama katika misingi ya malezi ya wazazi na kuleta maadili mazuri katika wanachuo ili kupata matokeo bora katika ufaulu wa wanafunzi hao.
“Ili kupata ufaulu mzuri katika masomo yenu na kuwa waadilifu katika kufikia malengo yenu muwapo chuoni lazima mjenge nidhamu ya hali ya juu ambayo ndio kitambulisho muhimu katika maofisini na kwenye taasisi zote ili kupata kizazi bora cha kulitumikia taifa letu” Ameongeza Dkt. Tego.
Dkt. Tego ameendelea kusema kuwa utendaji bora katika kufanya kazi unaendana sambamba na kusimamia maadili, kanuni, taratibu na sera za sehemu husika ili kufikia malengo yanayo takiwa katika sehemu husika.
Naye mmoja wa wanafunzi wa MUM ambaye hakutaka kutajwa jina lake ametoa wito kwa uongozi wa chuo kujenga utamaduni wa kuwa na vikao vya kitaaluma ili kuwajenga wanafunzi kisaikolojia na kuaandaa kuwa viongozi na watendaji katika nafasi tofauti hapa nchini kwani vijana ni nguvu ya taifa letu.

2 comments :

  1. naomba contact za Dr. Abdallah Yahya Tego, sababu kwa hapa kwetu Rwanda hatunaga hata one banki ya kiislam, so nataka niweze kuelimishwa zaidi. samahane mnipeni contact za Dr. Abdallah Yahya Tego

    ReplyDelete
  2. naomba contact za Dr. Abdallah Yahya Tego, sababu kwa hapa kwetu Rwanda hatunaga hata one banki ya kiislam, so nataka niweze kuelimishwa zaidi. samahane mnipeni contact za Dr. Abdallah Yahya Tego, mimi hupatikana kwenye +250788675459

    ReplyDelete