Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde akizungumza na wanafunzi wa Kidato Cha
Sita mkoani Simiyu walio katika kambi ya Kitaaluma katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa, wakati alipotembelea kambi hiyo Aprili
25,2019.
Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato Cha Sita
mkoani Simiyu wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde (hayupo pichani) wakati
alipowatembelea katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 25, 2019.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest
Hinju akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mtendaji wa Baraza la
Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde azungumze na wanafunzi wa
Kidato Cha Sita mkoani Simiyu, walio katika kambi ya Kitaaluma Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa Aprili 25, 2019.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa, Julieth John akitoa shukrani kwa Katibu
Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde
alipowatembelea Wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu, Aprili 25,
2019 katika kambi ya Kitaaluma Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa
Mwanafunzi wa Kidato Cha Sita Shule ya
Sekondari Simba wa Yuda, Innocent Leonard akitoa shukrani kwa Katibu
Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taiga(NECTA), Dkt. Charles Msonde
alipowatembelea Wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu, Aprili 25,
2019 katika kambi ya Kitaaluma Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana
Maswa, Mwl. Kuyunga Jackson akizungumza kwa niaba ya walimu wakati wa
ziara ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt.
Charles Msonde katika kambi ya Kitaaluma kwa Wanafunzi wa KIDATO Cha
Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 25, 2019.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde(katikati walioketi) akiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Idara ya Elimu Mkoa wa Simiyu, walimu
na wanafunzi wa Kidato Cha Sita mkoani Simiyu, Mara baada ya
kuhitimisha ziara yake katika kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi wa Kidato
cha Sita inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
…………………..
Na Stella Kalinga, Simiyu
Katibu MTENDAJI wa Baraza la Taifa la
Mitihani nchini (NECTA) amewataka wanafunzi wa kidato cha sita nchini
wanaotarajia kufanya mtihani wao wa mwisho mapema mwezi Mei, 2019
kuepuka
aina yoyote ya udanganyifu kwenye mtihani huo.
Dkt. Msonde ameyasema hayo wakati
akiongea na wanafunzi wa kidato cha sita mkoani Simiyu waliopo kwenye
kambi ya kitaaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, ambayo
inayohusisha wanafunzi 1166 kutoka shule 12 zikiwemo 10 za umma na mbili
za binafsi zenye kidato cha sita.
“Niwatake msifanye asilani habari
yoyote ya udanganyifu kwenye mtihani wenu, mkifanya hayo tu kwanza
yatawafanya mshindwe lakini pili tutakaponusa tu harufu yoyote ya
udanganyifu tutawafutia matokeo”alisema Dkt. Msonde.
Wakati huo huo Dot. msonde amewataka
wanafunzi hao kuondokana na dhana kwamba mtihani wa Taifa ni mgumu hali
inayopelekea kuwa na homa ya mtihani(hofu), badala yake wajiamini na
wajiandae vema kwa kuzingatia waliyofundishwa na walimu wao.
Pamoja na hayo amewapongeza viongozi
wa mkoa wa Simiyu kwa ubunifu wao wa kuanzisha kambi za kitaaluma hatua
inayopelekea mkoa huo kupiga hatua ya katika ufaulu wa mitihani ya
kidato cha sita na kidato cha nne.
Awali akimkaribisha Katibu Mtendaji wa
NECTA, Afisa Elimu mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema kuwa
awali mkoa ulikuwa na ufaulu mbaya lakini kupitia kambi ufaulu umepanda
kuanzia matokeo ya kidato cha sita kutoka nafasi ya 26 mwaka 2017 hadi
nafasi ya 10 mwaka 2018 na kidato cha nne kutoka nafasi ya 12 mwaka 2017
hadi nafasi ya 9 mwaka 2018.
Akiongea kwa niaba ya walimu mkuu wa
shule ya sekondari ya wasichana Maswa Mwl. Kuyunga Jackson amesema kuwa
vijana wa kidato cha sita Simiyu wamepikwa vizuri kitaaluma hivyo
matarajio yao ni kuingia tatu bora kitaifa.
Katika hatua nyingine wanafunzi
waliopo kambini hapo wamesema kuwa ujio wa katibu mtendaji NECTA umekuwa
chachu ya ufaulu wao na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote aliyoyaeleza
ikiwemo kuepuka udanganyifu pamoja na kuondoa homa ya mtihani.
“Tunakushukuru Sana kwa ujio wako
umetujenga na kutuondolea hofu ya mtihani, tutafanyia kazi uliyotueleza,
tunakuhakikishia hatutajihusisha na udanganyifu wowote kwa sababu
walimu wametuandaa vizuri na tunajua udanganyifu unaweza kusababisha
tusifikie ndoto zetu; tutazingatia yote tuliyofundishwa na walimu wetu”
alisema Julieth John.
No comments :
Post a Comment