Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto), Katibu
Tawala Msaidizi mkoa wa Arusha Miundombinu Mahmoud Mansour (kulia),
Mkurugenzi Mtendaji wa TANFOAM Riaz Lemtula (katikati) na Mshauri wa
TANFOAM Victor Njau wakijadiliana na namna ya kumega eneo kwa ajili ya
wafugaji wa kimasai wa kijiji cha Lengiroliti wilaya ya Monduli mkoa wa
Arusha wakati Waziri wa Ardhi alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina
ya kijiji hicho na Mwekezaji.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuviu akijadiliana na
wafugaji wa kimasai wa kijiji cha Lengiroliti wakati alipokwenda kutatua
mgogoro wa ardhi kati ya kijiji hicho na mwekezaji wa Shamba TANFOAM.
Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Lengiroliti Baraka Lemai.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na
wananchi wa vijiji vya Lengiroliti na Naaralami wilaya ya Monduli mkoa
wa Arusha alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya vijiji hivyo na
wawekezaji wa mashamba TANFOAM NA na SLUIS. Kulia ni Mkurugenzi wa
TANFOAM Riaz Lemtula (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).
………………………………………………………………………………….
Na Munir Shemweta, WANNM MONDULI
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemaliza mgogoro
uliodumukwa muda mrefu baina ya wananchi wa vijiji vya Lengiloriti na
Naalarami vilivyopo
wilayani Monduli mkoani Arusha na wawekezaji wa
mashamba yanayomilikiwa na TANFOAM na SLUIS kwa kuamua kumega sehemu za
mashamba na kuwapatia wananchi wa vijiji hivyo.
Lukuvi
alifikia umauzi huo baada ya kukutana na pande zote mbili jana tarehe
23 Aprili 2019 wilayani humo na kujadiliana kwa kina kwa takriban saa
tano kwa lengo la kupata suluhu ya mgogoro huo ambao umeleta sintofahamu
kati ya wananchi wa vijiji hivyo na wawekezaji wa mashamba.
Katika
makubaliano hayo iliamuliwa ekari kati ya 850 hadi 900 zimegwe kutoka
kwa muwekezaji TANFOAM na kugawiwa kwa kijiji cha Lengiloriti wilayani Monduli kutoka shamba namba 44 lenye ukubwa wa ekari
3098. Aidha, upande wa muwekezaji SLUIS jumla ya ekari 2000 za
muwekezaji zimetolewa kwa kijiji cha Naaralami, NAFCO, Lokisari na
Tukusi ambapo sasa muwekezaji atabaki na aekari 2217 badala ya 4,217
alizokuwa nazo awali.
Kwa
mujibu wa Lukuvi, ardhi iliyomegwa na kurudishwa katika vijiji hivyo
itakuwa chini ya mamlaka ya kijiji ambacho ndicho kitakuwa na jukumu la
kuigawa upya kwa wananchi wa vijiji husika na baadaye kupangwa matumizi
bora ya ardhi.
Akizungumzia
kijiji cha Lengiloriti, Waziri wa Ardhi aliwataka wananchi wenye Maboma
yaliyokuwa ndani ya eneo la shamba la muwekezaji TANFOAM kuhamia eneo
jipya walilotengewa katika kipindi cha miezi mitatu ili kupisha
muwekezaji kuendelea na shughuli za kilimo na kutotekelezwa kwa aina
yoyote agizo hilo kutaifanya serikali kuchukua hatua.
Maboma
yaliyohamishwa ni pamoja na linaloongozwa na mwenyekiti wa kijiji cha
Lengiloriti Baraka Lemai. Maboma mengine ni la Kaay Rao, Remi Paraleti,
Kelemo Kipara, Yamat Miriliali, Bete Kabulua, Barik Simon, Rais
Ramadhani, Ramadhani Hamis na Lakalai Olodo ambapo
Waziri wa Ardhi alisisitiza wamiliki wa Maboma hayo kupewa kipaumbele
wakati wa kugawiwa ekari zilizotolewa na kiasi kitakachobaki wapatiwe
wananchi wengine.
Aidha,
ameagiza kuanzia wiki hii timu ya upimaji ardhi mkoani Arusha iende
ktika eneo hilo kwa ajili ya kuweka mipaka/alama za kudumu ili
kuepuka uvamizi mwingine unaoweza kutokea na kuagiza wawekezaji na
wananchi wa vijiji vilivyopatiwa ekari hizo kuchangia fedha kwa ajili ya
upimaji ambapo muwekezaji na wananchi walikubali kutoa milioni tano kwa
ajili ya upimaji.
Kuhusu mgogoro wa muwekezaji SLUIS, Lukuvi alisema muwekezaji huyo amekubali kutoa
ekari 520 kwa kijiji cha Naaralami pamoja na ekari 300 kwa ajili ya
kupitishia mifugo ya wananchi wa kijiji hicho huku ekari 513 zikitolewa
kwa NAFCO, 366 kwa Lokisari na ekari 301 kwa kijiji cha Tukusi.
Lukuvi
alisema serikali inawaeshimu sana wawekezaji wa sekta ya ardhi kwa kuwa
wanalipa kodi inayosadia utoaji wa huduma za jamii huku wananchi nao
wakipata ajira na kusisisitiza kuwa wawekezaji wanaomiliki mashamba
kisheria serikali itawalinda na kuonya baadhi ya viongozi wa vijiji
kujigawia maeneo bila ya kushirikisha wananchi wa vijiji husika.
‘’Nimekuja
kusuluhisha mgogoro siyo kunyanganya wawekezaji mashamba, wawekezaji
wamekubali kupunguza mashamba yao na hayo mashamba siyo mali ya wananchi
wanaoishi katika maboma yaliyohamishwa bali ni mali ya kijiji ambacho
kitakuwa na jukumu la kugawa maeneo hayo’’ alisema Lukuvi
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa, baada ya
makubaliano ya pande zote mbili anategemea kila upande utaheshimu
maamuzi yaliyotolewa na mtu yoyote atakayekiuka basi serikali ya mkoa
itachukua hatua kali dhidi yake.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tanfoam Riaz Lemtula amepongeza jitihada iliyofanywa na
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi mpaka
kufikia muafaka wa suala hilo na kuahidi kutekeleza makubaliano
waliyoafikiana kwa lengo la kuleta maendeleo.
Naye
Mwenyekiti wa kijiji cha Lengiroliti Baraka Lemai alimshukuru Waziri wa
Ardhi kwa niaba ya Kijiji chake kwa kazi anayoifanya ya kutatua
migogoro ya ardhi na kuahidi kushirikiana na wawekezaji waiokubali
kumega maeneo yao kwa ajili ya kijiji.
Wawekezaji
wanaomili mashamba katika vijiji hivyo wamekuwa wakiendesha mashamba
yao katika shughuli za kilimo ambapo hulima mazoa ya Maharage, Mtama,
Ngwara na mahindi na kusafirisha mazo hao katika nchi za Sweden, Canada
na Uholanzi.
No comments :
Post a Comment