Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia), Mkuu wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, wakisaini Mkataba wa
Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, katika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Ujenzi wa Jengo hilo ambalo litakua na
ghorofa nane unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 18. Katibu Mkuu
ameitaka Suma JKT kumkabidhi jengo hilo kwa wakati.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza na Maafisa wa
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na wa Wizara yake, kabla ya kusaini Mkataba
wa ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, jijini Dodoma, leo. Suma
JKT wanatarajia kujenga jengo hilo ambalo litakua na urefu wa ghorofa
nane, na litakamilika baada ya miezi 18. Kushoto meza kuu ni Mkuu wa
Jeshi hilo, Meja Jenerali Martin Busungu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kushoto), akimuaga Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taida (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, mara
baada ya kumaliza kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya
Uhamiaji, jijini Dodoma, leo. Suma JKT wanatarajia kujenga jengo hilo
ambalo litakua na urefu wa ghorofa nane, na litakamilika baada ya miezi
18
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (watatu kushoto), Mkuu wa Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu (watatu kulia),
wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa JKT na Wizara, mara baada ya
kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Makao
Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Ujenzi wa Jengo hilo ambalo
litakua na urefu wa ghorofa nane unatarajiwa kukamilika baada ya miezi
18. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………………..
Na Mwandishi Wetu, MOHA
KATIBU Mkuu wa Wizara Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu amelitaka Shirika la Uzalishaji
Mali Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT), kujenga jengo la Makao Makuu ya
Idara ya Uhamiaji kwa ufanisi mkubwa na akabidhiwe jengo hilo baada ya
miezi 18.
Akizungumza kabla ya kusaini
mkataba wa makubaliano wa ujenzi wa jengo hilo, kati ya Wizara yake na
Suma JKT ambayo iliongozwa katika kikao hicho na Mkuu wa JKT, Meja
Jenerali Martin Busungu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo,
iliyopo Mji wa Serikali, Kata ya Mtumba, jijini Dodoma, leo, alisema
hana shaka na uwezo wa Mkandarasi huyo, ila anaamini ujenzi huo utakua
bora na utakamilika kwa wakati.
“Baada ya maandalizi ya ujenzi huu
kuchukua muda mrefu lakini hatimaye tumekamilisha, hivyo nawaomba ndugu
zangu tufanye kazi vizuri kabisa, na leo ndio siku ya kusaini mkataba
kwa ajili ya ujenzi huu,” alisema Meja Jenerali KIngu.
Meja Jenerali Kingu alisema Wizara
yake itafuatilia kwa karibu ujenzi huo, ambapo Mkandarasi ni Suma JKT
na Mshauri Elekezi ni Chuo Kikuu cha Ardhi, hivyo jengo hilo anatarajia
kuwa bora zaidi kutokana na uwepo wa wadau hao.
Kwa upande wake, Mkuu wa JKT, Meja
Jenerali Busungu, alisema aliishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
kwa kuwa na imani na Suma JKT na kuipa kazi ya ujenzi wa jengo la makao
makuu ya uhamiaji jijini Dodoma.
“Tunaishukuru Wizara yako kwa
kutupa kazi hii ya ujenzi wa jengo hili ambalo ni la ghorofa nane,
tunaahidi kulikamilisha baada ya miezi 18, na tutapiga kadiri
inawezekana, tupo tayari kwa kazi yenye uweledi wa kuzingatia muda na
ubora ambao utawauza zaidi Suma JKT,” alisema Meja Jenerali Busungu.
Mkataba huo ulisainiwa na viongozi
hao huku ukishuhudiwa na wanasheria wa taasisi hizo ambao ni Mkurugenzi
wa Sheria, Marlin Komba wa Wizara hiyo na Kapteni Joyce Mwaikofu kutoka
JKT.
No comments :
Post a Comment