Kamati ya Bunge, Mifugo, Kilimo na
Maji imempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro
kutokana na mkakati wake wa kukwama miradi ya maji iliyokwama kwa muda
mrefu katika wilaya hiyo.
Hayo yamejiri kwenye ziara ya
kamati hiyo wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya kamati ya Bunge
Mifugo, Kilimo na Maji kufanya ziara yakukagua miundo mbinu ya miradi
mikubwa ya maji ya vijiji 10 inayoendelea kujengwa yenye lengo la
kuondoa changamoto ya
uhaba wa maji safi na salama .
Akizungumza mara baada ya kukagua
Miradi hiyo ya Maji Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,
Eng. Emmanuel Kalobelo amesema amefurahishwa na kitendo cha Mkuu wa
wilaya ya Arumeru Ndugu Muro ya kuwasaidia wakandarasi kupata vifaa vya
ujenzi yakiwemo mabomba makubwa ya maji kwa dhamana ya ofisi yake kwa
wenye viwanda uku taratibu za malipo zikiendelea hatua inayosaidia
miradi hiyo kukamilika kwa wakati
“Nashukuru kwa maelezo ya Mhe.
Mkuu wa Wilaya ambaye tangu asubuhi ameonyesha jinsi gani anavyofuatilia
miradi yote ndani ya wilaya yake, na anafahamu takwimu zote za miradi
na stegi zilizofikiwa hivyo Mimi kama mtu wa sekta ya maji nimefarijika
kweli na uongozi wa Wilaya ya Arumeru.” Alisema Naibu Emmanuel Kalobelo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
kamati hiyo ya bunge Ndugu Mahamoud Mgimwa amesema DC Muro anaitaji
pongezi na kuungwa mkono kutokana na juhudi zake anazoonyesha
zakuwaletea wananchi wake maendeleo kwa kufuatilia miradi kila hatua ,
pamoja na kuhakikisha wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya miradi
wananufaika kwanza *, hatua ambayo amesema inadhihirisha kuwa *Dc Muro
hakai ofisini na badala yake anatumia muda mwingi katika kutembelea
miradi
“Mhe Muro hapa anafanya kazi nzuri
kuna kazi nyingine ambazo so za kwake lakini anajitolea,naomba
tumpongeze sana, unawezajiuliza anafanya kwa ajili ya nani? Lakini
ameamua kufanya kwa ajili ya kuwasaidia nyinyi ndugu zake, kwa zile
juhudi anazozifanya mkuu wa wilaya na waombeni sana mumuunge mkono.”
Alisema Mahamoud.
Kamati hiyo pia ilipata fursa ya
kutembelea Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji * mifugo kwa njia ya chupa
NAIC Kilichopo Wilayani Arumeru. ambapo walijionea kazi zinazofanywa za
kutengeneza mbegu za Ng’ombe wa kisasa wa maziwa na nyama .
No comments :
Post a Comment