Wakili wa Kujitegemea Godfrey
Wasonga,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini
Dodoma wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais wa Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS) .
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
…………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wakili wa Kujitegemea Godfrey
Wasonga ametangaza kugombea nafasi ya Urais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika (TLS) amesema kuwa endapo atachaguliwa atafanya ushawishi wa
kubadilisha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dodoma amesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais wa
TLS mojawapo ya jambo ambalo atalipigania ni kuhakikisha anatumia nafasi
yake kufanya ushawishi wa kubadilisha katiba ya Tanzania ili kuondoa
sheria kandamizi.
“Kwa sasa hakuna demokrasi ya
kweli kutokana na kuwepo kwa katiba iliyopitwa na wakati
ambayo
haiendani na matakwa ya kidunia ya sasa”amesema Wasonga.
Aidha Wakili Wasonga amesema kuwa
ikumbukwe kuwa katiba tuliyonayo kwa sasa niyamwaka 1964 ,ambayo
ilifanyiwa marekebisho mwaka 1977 hivyo kwa sasa haiwezi kuendana na
matakwa ya kidunia
Wakili huyo amesema kuwa kama
hakuna katiba yenye kurekebishwa na kuondoa sheria kandamizi nchi
haiwezi kuwa na demokrasia ya kweli na ikiwepo katiba nzuri itaweza
kumsaidia hata rais aliyepo madarakani.
Hata hivyo Wasonga amesema kuwa
iwapo atapata nafasi ya kuwa rais atakuwa na vipaumbele vitano ambavyo
ni kubadilisha katiba ya TLS kutoka kufanya uchaguzi kwa mwaka mmoja na
kuwa miaka miwili.
“Endapo nitachaguliwa pia
nitaboresha huduma kwa wanachama hasa katika bima ya Afya ili kila
wakili awe na bima ya afya ambayo itaweza kumsaidia yeye na familia
yake”alisisitiza
“Pia nitakiondoa kipengele cha
ulipaji wa ada ambayo hulipwa kila mwisho wa mwaka na badala yake iwe
inalipwa mwanzo wa mwaka au wakati wowote na siyo lazima mwisho wa
mwaka”amesema Wasonga
Wakili Wasonga amesema kuwa katika
uongozi wake atakuwa na sera ya pensheni kwa mawakili ambao watakuwa
wamefikia uzeeni ili wawe na kitu ambacho kitaweza kuwasaidia.
“Ada za mawakili zimekuwa
zikiongezeka kutoka sh.30000 hadi kufikia sh.50000 , na ili uweze kufika
katika vikao vya mawakili ni lazima ulipe kiasi cha sh.120,000 lakini
katika uongozi wangu nitaishusha hadi kufikia kiasi cha sh. 60000 kama
ilivyokuwa awali ili kumpunguzia mwanachama badala ya kumuongezea
gharama.
Hata hivyo Wasonga amesema kuwa
katika uongozi wake atatoa elimu juu ya ujasiriamali ambao utaweza
kumsaidi wakili pale ambapo hatakuwa na kazi.
Amesema kuwa wapo Mawakili
wachanga ambao wanahitaji kuboreshewa mazingira ikiwa ni namna gani ya
kuweza kuwapatia mikopo yenye riba nafuu katika mabenki au akiwa
mwanachama anaweza kukopeshwa moja kwa moja kutoka katika mfuko wa chama
cha Mawakili.
Aidha amesema kuwa kumekuwepo kwa
mahusiano mabaya kati ya TLS, Serikali na Bunge,hivyo endapo
atachaguliwa anategemea kupata mahusiano mazuri kati ya mihilimi hiyo.
Hata hivyo Wasonga amesema kuwa
mchakato wa kuanza harakati za kutafuta kura utaanza Machi 13 na
uchaguzi unatarajiwa kufanyika mnamo April 6 mwaka huu.
No comments :
Post a Comment