Tuesday, March 12, 2019

MKURUGENZI WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA NGUVU ZA ATOMU (IAEA) KANDA YA AFRIKA KUTEMBELEA ZANZIBAR


Prof-Shaukat-A.-Abdulrazak-1
Arusha, 12
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (IAEA) kanda ya Afrika Profesa Shaukat  Abdulrazak anatarajia kuonana na viongozi mbali mbali wa Serikali ya  Mapinduzi ya Zanzibar Marchi 13.
Mkurugenzi huyo ataambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Tume  ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Lazaro Busagara ambao watapata nafasi ya kufanya mazungumzo na
viongozi mbali mbali.
Mkurugenzi huyo aliweza pia kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa kimataifa  wa waratibu (NLOs) wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia unaowahusisha  nchi wanachama 46 wa Shirika la Nguvu za Atomu Duniani uliofunguliwa March 11 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha unaoendelea jijini Arusha.
Shirika la Nguvu za Atom duniani IAEA linatoa ufadhili kwa serikali ya Tanzania katika miradi mbali mbali  inayohusisha sekta za Afya, Kilimo, Maji, Mifugo, Rasilimaliwatu, Nishati na Viwanda ambapo mpaka sasa ni jumla ya  shilingi za kitanzania bilioni 9.5 zimetolewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na gharama za mafunzo kwa wataalamu katika masuala ya afya.

No comments :

Post a Comment