Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI Mhe.Selemani Jaffo
akizungumza na Maafisa Utamaduni wa mikoa na Halmashauri zote nchini
(hawapo katika picha) wakati akifunga Kikao Kazi cha Sekta hiyo
kilichofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawi. Akizungumza na Maafisa
Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini (hawapo katika picha)
wakati akifunga Kikao Kazi cha Sekta hiyo kilichofanyika kwa siku mbili
Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Maendeleo ya Utamaduni Bw.Boniface Kadili akitoa maelezo mafupi kuhusu
ya Sekta yake wakati wa ufungaji wa Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni wa
Mikoa na Halmashauri zote nchini kilichofanyika kwa siku mbili Jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI Mhe.Selemani Jaffo
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Maafisa Utamaduni wa
mikoa na Halmashauri zote nchini baada ya kufunga Kikao Kazi cha Sekta
hiyo kilichofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
…………………..
Na Shamimu Nyaki -WHUSM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Seleman Jaffo
amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote
nchini kuwawezesha Maafisa Utamaduni kwa kuwaongezea Bajeti
itakayowawezesha kutimiza majukumu yao kwa ufasaha.
Agizo hilo amelitoa leo Jijini
Dodoma wakati alipokuwa akifunga Kikao Kazi cha 11 cha
Maafisa
Utamaduni kilichofanyika kwa siku mbili ambapo amewaagiza Wakurugenzi
kutambua majukumu ya maafisa Utamaduni ikiwemo kuhifadhi kuendeleza
mila na desturi pamoja na kukuza lugha ya kiswahili.
“Sekta hii ni muhimu sana kwakua
ina wajibu wa kuelimisha na kuburudisha,hivyo naendelea kuwasitiza
Wakurugenzi kuwawezesha Maafisa Utamaduni kushiriki katika kila
Mkutano,kongamano,warsha zote zinazohusu sekta hiyo”.Alisema Mhe. Jaffo.
Aidha ameongeza kuwa thamani ya
maafisa Utamaduni ni lazima ionekane kwakua ndio tasnia inayofundisha na
kukuza Uzalendo hasa kujua alama,nyimbo na tunu za Taifa kwa vijana na
wanafunzi nchini.
Katika hatua nyingine Mhe.Jaffo
amewahakikishia Maafisa Utamaduni kuwa wavumilivu kuhusu muundo wa Kada
hiyo ambapo amewaahidi kuwa suala hilo limepokelewa na Serikali itaanza
mchakato wake ili kutatua changamoto hiyo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi amesema kuwa
Kikao Kazi hicho ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Utamaduni ya mwaka
1997 inayoeleza kuwa Wasimamizi na Watendaji wakuu wa shughuli za
Utamaduni katika ngazi ya Taifa, Mkoa Wilaya na Taasisi za elimu na
mafunzo kupata mafunzo ya uendeshaji ili kuwawezesha kutekeleza majukumu
yao.
“Kikao Kazi hiki kimepitisha
maazimio yatakayokuwa mwongozo katika kuboresha utendaji wa Sekta hii
ili kuimarisha utendaji kazi Ki-muundo na kisera baina ya maafisa
Utamadduni wote waliopo Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI”.Alisema Bibi Susan.
Naye Afisa Utamaduni Wilaya ya
Urambo Bw.Tito Lulandala ameeleza kuwa Sekta ya Utamaduni ina fursa
nyingi zinazoweza kukuza pato la mwananchi mmoja na Taifa kwa ujumla
katika nyanja mbalimbali ikwemo Michezo Sanaa na kukuza Utalii.
Katika kikao kazi hicho mada
mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo Umuhimu wa Ubidhaishaji wa lugha ya
kiswahili,Uhuishaji wa Sera ya Utamaduni,Sekta ya Filamu nyenzo muhimu
katika kuimarisha Asili na Utamaduni
,Fursa za utalii wa Kiutamaduni na nyinginezo.
No comments :
Post a Comment