Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji (MB) akiwa na mwenyeji wake Makamu Mkuu wa Chuo sili Chuo
Pro. Lughano Kusiluka; baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe; alipofanya
ziara hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akiweka saini kwenye kitabu cha Wageni
baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
akiwasili eneo la Maekani ambako ujenzi wa mabweni ya wanafunzi
unaendelea. Kushoto ni Prof. Ernest Kihanga Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo
Utawala na Fedha, akifuatiwa na Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB), mwenye
kofia ni injinia na msimimizi ya mradi Injinia Focus Alex Odecho, na wa
mwisho kulia ni Prof. Lughano Kusiluka Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akielekeza jambo kwenye moja wapo ya
majengo ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea eneo la Maekani.
Kulia ni msimamizi wa mradi Injinia Focus Alex Odecho.
Bi. Amina Jumanne Mkazi wa kipera
ambaye ni kibarua katika ujenzi unaoendelea eneo la Maekani akisaliana
na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) wakati
alipotembelea shughuli ya Ujenzi inayoendelea.
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB)
afurahia zawadi yenye kumbukumbu ya Chuo Kikuu Mzumbe alichosoma na
kufanya kazi kabla ya kuingia kwenye siasa.
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
(katikakati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu
Mzumbe alipotembelea hivi karibuni.
………………………..
Naibu Waziri Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) ametembelea Chuo Kikuu Mzumbe na kukagua
ujenzi wa Mabweni ya Wanafunzi unaoendelea katika eneo la Maekani, Makao
Makuu ya Chuo hicho, Morogoro.
Mhe. Naibu Waziri, amepongeza
jitihada kubwa zilizofanywa na Uongozi wa Chuo kwa kushirikiana na
Serikali katika kutatua kero ya malazi kwa wanafunzi na kusisitiza
umuhimu wa kuanza mara moja awamu ya pili ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa na mihadhara katika
eneo hilo ili kuwarahisishia wanafunzi
kutotembea umbali mrefu wakati wa masomo.
“Serikali inategemea mchango
mkubwa wa Vyuo Vikuu katika kutimiza malengo; hasa kwenye hili la ukuaji
wa uchumi. Pamoja na kwamba tunajivunia uchumi wetu kukua lakini
tusibweteke, badala yake tufanye tafiti na kuandaa vema vijana ambao
watakuwa watumishi bora wa Umma wanaoendana na dhana ya sasa ya nidhamu
ya kazi. Hivyo, nimefarijika sana kuona maendeleo na hatua kubwa ambayo
mmepiga kitaaluma na katika miradi ya maendeleo mnayosimamia” alisema
Mhe. Naibu Waziri.
Akikamkaribisha Naibu Waziri
huyo, ambaye pia alipata fursa ya kuzungumza na Menejimenti ya Chuo
Kikuu Mzumbe; Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka amemweleza
Mheshimiwa Naibu Waziri kuwa, kwa sasa Chuo Kikuu Mzumbe kinatekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo ya miundombinu katika Kampasi Kuu ya
Morogoro, Kampasi ya Mbeya na Kampasi ya Dar-es-salaam na kwamba, lengo
ni kuendelea kutumia ruzuku inayotolewa na Serikali na vyanzo vya mapato
ya ndani kuendeleza ujenzi na kuboresha miundombinu ya Chuo ili kujenga
mazingira bora ya utoaji wa Elimu ya Juu.
“Napenda kuipongeza sana
Serikali yetu kwa kutambua mchango mkubwa wa Vyuo Vikuu nchini, na kwa
upande wa Taaluma, Chuo chetu kitaendelea kuunga mkono jitihada za
Serikali ya Awamu ya Tano katika kuendeleza Uchumi wa Viwanda; kwa
kuendelea kufanya tafiti, kubuni miradi ya maendeleo na kutoa nguvu kazi
itakayowezesha Tanzania kufikia malengo yake” alisema Prof. Kusiluka.
Ameahidi Chuo Kikuu Mzumbe
kuendelea kuimarisha uhusiano na kufanya kazi kwa karibu zaidi na
Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Umma kwa kubadilishana ujuzi na
uzoefu, pamoja na kutumia wanataaluma kuboresha utendaji Serikalini,
kulinda nidhamu na kuinua kiwango cha elimu inayoendelea kutolewa na
Chuo hicho.
Mradi wa Ujenzi wa Mabweni
katika Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu Mzumbe ambao unafadhiliwa na
Serikali,unatekelezwa na SUMA JKT na unategemewa kukamilika ifikapo
mwezi Oktoba mwaka huu. Mradi unategemea kugharimu kiasi cha shilingi
bilioni 6.5 hadi utakapokamilika. Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha
wanachuo wengi zaidi katika Kampasi Kuu kukaa kwenye hosteli za Chuo.
No comments :
Post a Comment