Friday, March 1, 2019

MAANDALIZI YA UJENZI WA KABURI AMBALO UTAHIFADHIWA MWILI WA MAREHEMU RUGE MUTAHABA YANAENDELEA


1
Maandalizi ya Shughuli ya Mazishi ya Ruge Mutahaba yanaendelea Nyumbani Kwao Kabale, Bukoba ambapo ndipo Mwili utakapostiriwa.
Ujenzi wa Kabuli unaendelea kwa kasi ambapo Fundi anathibitisha kufikia jioni Leo litakuwa limekamilika ukiwa unasubiriwa mwili ambao utawasili jijini Dar es salaam leo kwa ndege ukitokea Afrika Kusini ambako ndiko alikokuwa akipokea matibabu.
Baada ya kuwasili jijini Dar es salaam Saa tisa arasili leo mwili wa marehemu Ruge utapitishwa katika barabara za Nyerere, Mandela, Buguruni, Karume, Magomeni, Moroco Hotel, Sinza Kijiwezi, Bamaga, ITV, Clouds ambapo utaingizwa kwa muda mfupi katika ofisi za Clouds na kufanya sala kidogo na kisha kuondoka kupitia barabara ya Kawe na baadaye barabara ya Mwenge kisha Utapelekwa katika Hospitali ya Jeshi a Wananchi Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa
Kesho Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba utapelekwa katika viwanja vya Karimjee na kuagwa na viongozi mbalimbali, Wasanii Ndugu, Jamaa Marafiki na waombolezaji mbalimbali na kisha kusafirishwa kwa ndege  kurelekea mkoani Kagera siku ya jumapili ambapo utazikwa siku ya Jumatatuo Nyumbani Kwao Kabale, Bukoba.
Vikao vya kamati vinaendelea kila Mara kuhakikisha shughuli inakwenda kama ilivyopangwa ingawa Kuna uwezekano wa Shughuli ya kuaga na salaam za mwisho ikafanyika uwanjani sehemu nyingine kutokana na ufinyu wa eneo la Nyumbani eneo la mazishi.
3
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kaburi.
4
Baadhi ya kamaburi ya wanafamilia waliozikwa eneo hilo.

No comments :

Post a Comment