Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst)
George Mkuchika (Mb), akisalimiana na Balozi wa
Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke alipowasili Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania kukabidhi kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst)
George Mkuchika (Mb), akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya
kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye
ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo akitoa neno la utangulizi
wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo chake
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini
Dar es Salaam.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China
nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza kabla ya kukabidhi kompyuta kwa
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakati wa hafla fupi
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania (TPSC), Dkt. Charles Msonde.
Baadhi ya watumishi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst)
George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) katika hafla fupi ya makabidhiano
ya kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye
ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst)
George Mkuchika (Mb) akimkabidhi zawadi Balozi wa
Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke baada ya hafla fupi ya
makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst)
George Mkuchika (Mb) akipokea moja ya kompyuta mpakato kutoka kwa
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke katika hafla
fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi, Dkt. Laurean
Ndumbaro.
……………………….
Serikali ya Tanzania imeishukuru
China kwa kuipatia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kompyuta
mpakato 20 zitakazowasaidia katika shughuli za ufundishaji na kuboresha
utendaji kazi kwa watumishi wa chuo hicho.
Akipokea kompyuta hizo kutoka kwa
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) amemshukuru Balozi huyo kwa mchango wao katika kuboresha Chuo hicho kwa maendeleo ya taifa.
Mhe. Mkuchika amepongeza
ushirikiano ambao China imekuwa nao kwa Chuo cha Utumishi wa Umma katika
masuala mbalimbali ya kuboresha utendaji ikiwa ni pamoja na watumishi
wa chuo hicho kushiriki semina mbalimbali nchini China ambazo
zinawasaidia kuongeza ujuzi.
Ameomba ushirikiano huu uzidi
kudumu kwani China imekuwa na mahusiano mazuri na Tanzania kwa muda
mrefu sasa tangu Serikali ya awamu ya kwanza mpaka sasa.
Pia, Mhe. Mkuchika amemuomba
Balozi huyo kusaidia katika ujenzi wa tawi jipya la chuo hicho
linalotarajiwa kujengwa jijini Dodoma baada ya Serikali kuhamishia
shughuli zake Makao Makuu ya nchi Dodoma na kuongeza kuwa ujenzi wa chuo
hicho utatoa fursa kwa watumishi waliohamia Dodoma na mikoa jirani
kuongeza ujuzi katika Chuo hicho.
Akikabidhi kompyuta hizo, Balozi
Wang Ke amesema, lengo lao ni kuboresha utendaji kazi wa watumishi
katika chuo hicho hususan katika kufundisha.
Balozi Wang Ke amefafanua kuwa,
anatamani kukiona Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kikitoa elimu bora
zaidi na kikizalisha watumishi wa umma bora nchini.
Aidha, Balozi Wang Ke ameahidi
kuendeleza ushirikiano ulioanza kati ya Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania na vyuo vya mafunzo vilivyoko nchini China ili kukuza
ushirikiano zaidi na kuendeleza utamaduni wa kujifunza baina ya Tanzania
na China.
Hafla hiyo imefanyika katika
ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na maafisa kutoka ubalozi wa China nchini Tanzania
wakiongozwa na Balozi Wang Ke, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi na
baadhi ya watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania.
No comments :
Post a Comment