Kikundi cha ngoma za asili kikitoa
burudani kabla ya Mkutano wa Mawaziri wa Bonde la Mto Zambezi (ZAMCO)
kuanza mkutano huo unalenga kujadili mpango mkakati wa miaka 20 kwa
Bonde la Mto Zambezi, na unashirikisha Mawaziri kutoka nchi nane
Wanachama wa ZAMCO, yaani Angola, Botswana, Malawi, Msumbiji,Tanzania,
Zambia na Zimbabwe uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa
Julius Nyerere kuanzia Februari 26 mpaka Februari 28.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maji
Shirikishi kimataifa Sylivester Matemu akitoa utambulisho kwa Mawaziri
wa nchi wanachama wa ZAMACO (hawapo pichani) katika Mkutano wa Mawaziri
wa Bonde la Mto Zambezi (ZAMCO) unaolenga kujadili mpango mkakati wa
miaka 20 kwa Bonde la Mto Zambezi, na unashirikisha Mawaziri kutoka nchi
nane wanachma za ZAMCO uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
kimataifa Julius Nyerere kuanzia Februari 26 mpaka Februari 28.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Prof. Makame Mbarawa akitoa hotuba ya kufungua mkutano wa Mawaziri wa
Bonde la Mto Zambezi (ZAMCO) unaolenga kujadili mpango mkakati wa miaka
20 kwa bonde la mto Zambezi, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
kimataifa Julius Nyerere kuanzia Februari 26 mpaka Februari 28.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Prof. Makame Mbarawa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawaziri wenzake
pamoja na watendaji wengine wa ZAMCO kutoka Nchi Wanachama mara baada ya
kufungua mkutano huo unaolenga kujadili mpango mkakati wa miaka 20 kwa
bonde la mto Zambezi, uliofanyika katika Kitu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Prof. Makame Mbarawa akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
mara baada ya kufungua mkutano wa Nchi Wanachama wa ZAMCO, unaolenga
kujadili mpango mkakati wa miaka 20 kwa bonde la mto Zambezi,
uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa Julius Nyerere
kuanzia Februari 26 mpaka Februari 28.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa
Nchi Wanachama wa ZAMCO wakifuatilia mkutano wa ZAMCO, unaolenga
kujadili mpango mkakati wa miaka 20 kwa bonde la mto Zambezi,
uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa Julius Nyerere
kuanzia Februari 26 mpaka Februari 28.
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO).
………………….
Abraham Nyantori
MAELEZO, Dar Es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Profesa Makame Mbarawa, amefungua Mkutano wa Saba wa Mawaziri wa Maji
wa nchi nane zilinazohusiana na Bonde la Mto Zambezi (Zambezi
Watercourse Commission – ZAMCOM) na kuitaka jamii ya mataifa hayo kuona
umuhimu wa
kamisheni ya chombo hicho kuendelea kuimarika na kusimamia
raslimali za ZAMCOM kwa manufaa yaliyokusudiwa.
Waziri Mbarawa alikuwa anafungua
kikao cha Baraza la Mawaziri wa Maji katika Ukumbi wa Mikutano ya
Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, vikao vikiwa ni
Mkutano wa Sita wa Baraza la Mawaziri Februari 26 – 27 na Mkutano wa
saba wa Kamati ya Wataalaam ya ZAMCOM, nchi husika zikiwa ni Angola,
Botswana, Msumbiji, Malawi, Namibia, Zambia, Zimbambwe na Mwenyeji
Tanzania.
Mkataba wa Kamisheni ya Bonde la
Mto Zambezi ulianza rasmi mwaka 2011 kwa lengo la kusimamia raslimali za
maji za Bonde la Mto Zambezi, Tanzania ambayo ni mwanachama maji yake
toka Ziwa Nyasa, kwa wastani wa asilimai 16 ya maji yaingiayo Ziwa
Zambezi kwa mito, humwagika Ziwa Zambezi na Bonde hilo linahitaji
hifadhi na zipo fursa za kuwepo miradi ya manufaa kwa nchi hizo.
Baraza limepokea Mpango kazi
(Strategic Plan) na Mfumo wa kubadilishana, kutumia na kuhifadhi
takwimu za raslimali za Maji kwa njia ya TEHAMA, ambapo Tanzania
imemaliza muda wake wa Uenyekiti na nafasi hiyo kupewa Zambia.
No comments :
Post a Comment