Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George
Mkuchika (Mb) akizungumza na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Mkwanyule
wilayani Kilwa katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya
msingi Mkwanyule wilayani humo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa
Mhe. Christopher Ngubiagai.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe.
Christopher Ngubiagai akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George
Mkuchika (Mb), kuzungumza na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Mkwanyule
wilayani Kilwa (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika kwenye
viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani humo.
Wakazi wa kijiji cha Mkwanyule
wilayani Kilwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika
(Mb) (hayupo pichani) katika mkutano wa Waziri huyo na wanufaika wa
TASAF uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani
Kilwa.
Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini,
Mhe. Selemani Bungara akiishukuru serikali kwa kuufikisha Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini wilayani kwake wakati wa mkutano kati ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na wanufaika wa TASAF uliofanyika
katika viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani humo.
Mmoja wa wanufaika wa TASAF mkazi
wa kijiji cha Mkwanyule Bi. Mwanahamisi Ally Ukwenda akishuhudia namna
alivyonufaika na TASAF wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt
(Mst) George Mkuchika (Mb) na wanufaika wa TASAF uliofanyika katika
viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani Kilwa. Kushoto kwake ni
mnufaika mwenzie Bi. Atili Masoud Swalehe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George
Mkuchika (Mb) (kulia) akikagua mradi wa mbuzi unaomilikiwa na Bw. Hassan
Charahani (kushoto) mara baada ya kumaliza mkutano kati yake na
wanufaika wa TASAF uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi
Mkwanyule wilayani Kilwa.
……………………………………………………………………………………..
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst)
George Mkuchika (Mb) amepongeza jitihada za Wanufaika wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa za
kujikwamua kiuchumi kwa kutumia vizuri fedha za TASAF.
Pongezi hizo amezitoa wakati wa
mkutano kati yake na wakazi wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa
uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani humo.
Mhe. Mkuchika ametoa pongezi hasa
kwa kinamama kwa kutumia vizuri fedha hizo katika kuzalisha miradi ya
maendeleo na amefurahishwa na ushuhuda wa akina mama ambao mwanzoni
walitumia vibaya fedha hizo lakini baadae wakawekeza katika miradi ya
maendeleo.
Mhe. Mkuchika ametoa ufafanuzi
kuwa lengo la kuanzishwa kwa TASAF ni kupambana na umaskini ili
kuboresha hali duni za Watanzani na kuagiza wanufaika wa TASAF
kutofanyia mzaha fedha wanazozipata.
Aidha, Mhe. Mkuchika amepongeza
wasimamizi wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa akiwemo Mkuu
wa Wilaya, Mkurugenzi na Mratibu wa TASAF wa halmashauri hiyo kwa
kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Akitoa ushuhuda katika mkutano
huo, mmoja wa wanufaika wa TASAF mkazi wa kijiji cha Mkwanyule, Bi.
Mwanahamisi Ukwenda, ameishukuru serikali kwa kuianzisha TASAF kwani
imemuwezesha kufanya shughuli za ufugaji wa kuku na mbuzi na kupata
fedha ambazo zinamsaidia kwa mahitaji maalumu mara anapouza mifugo hiyo.
Aidha, Bi. Mwanahamisi amekiri
kutotumia vizuri fedha za TASAF alizozipata katika awamu ya kwanza na ya
pili na kuahidi kuendelea kuzitumia vizuri fedha hizo kwa sasa.
Mnufaika mwingine, Bw.Hassan
Charahani ameushukuru mradi wa TASAF kwa kumkwamua kwenye umaskini kwani
hapo awali alikuwa akila mlo mmoja kwa siku na hakuweza kusomesha
watoto lakini TASAF imebadili maisha yake.
Kwa upande wake Mbunge wa Kilwa
Kusini, Mhe. Selemani Bungara ameishukuru serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha wakazi wa kijiji cha Mkwanyule kuwa
na miradi ya ufugaji kuku, mbuzi na kujenga bwawa la maji na pia
ameipongeza serikali kwa kutokua na ubaguzi katika kuleta maendeleo
nchini kwa kuwa Mkwanyule inaongozwa na viongozi wa chama cha CUF.
Mhe. Mkuchika anaendelea na ziara
ya kikazi mkoani Lindi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi wa umma pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
mkoani humo.
No comments :
Post a Comment