Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya
Musoma Bi. Vicky Mbunde akifungua kikao cha Kamati ya Ulinzi wa Wanawake
na Watoto ya Mkoa wa Mara kilichofanyika leo Mjini Musoma.
Katibu Tawala msaidizi Utawala na
Rasilimali Watu mkoa wa Mara Bi. Clothilde Komba akilezea umuhimu wa
kikao cha Kamati ya Mkoa ya ulinzi wa Wanawake na Watoto kilichofanyika
leo Mjini Musoma.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Sebastian
Kitiku akielezea umuhimu wa jumbe katika kuleta hamasa kwa jamii katika
kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kikao
kilichofanyika leo mjini Musoma.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa
Mara Bi. Neema Ibamba akieleza mikakti ya mkoa wa Mara katika kutekelza
Mpango wa Kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto
katika kikao kilichowakutanisha kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto
mkoa wa Mara.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.
Mathias Haule akielezea umuhimu wa uwepo wa Kamati ya Ulinzi kwa
Wanawake na Watoto kwa Kamati ya Mkoa wa Mara katika kikaokilichofanyika
leo mjini Musoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi kwa Wanawake na Watoto mkoa wa Mara wakifuatilia mada ,balimbali
zizilokuwa zikitolewa katika kikao hicho kilichofanyika mkoani
humo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
…………….
Na Mwandishi Wetu Mara
Mkoa wa Mara umeweka Mipango
dhatiti katika kuhakikisha wanapambana na vitendo vya kikatili dhidi ya
Wanawake na Watoto kwa kuhakikisha wanaifikia jamii katika kutoa ujumbe
sahihi wa kuaondokana na vitendo vya kikatili hasa vitendo vya ukeketaji
vilivyoshamiri
mkoani humo.
Hayo yamebainika leo mkoani Mara
wakati wa kikoa cha wadau kutoka Kamati ya Ulinzi ya Wanawake na Watoto
pamoja na wawakilishi wa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Mara kwa lengo
la kupokea jumbe mbalimbali zitakazosaidia kuelimisha jamii ya mkoa huo
kuondokana na mila potofu zinozopelekea vitendo vya kikatili kwa
wanawake na watoto.
Akifungua kikao hicho Mwakilishi
wa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Bi. Vicky Mbunde amesema kuwa kwa Mkoa wa
Mara kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013 vitendo vya ukatili wa kijinsia
vilikuwa asilimia 72 na vimepungua kufikia asilimia 66 mwaka 2015/2016.
Ameongeza kuwa tatizo la vitendo
ya ukatili mkoa wa Mara sio vya kutengenzwa bali kwa kiasi kikubwa
matatizo hayo husababishwa na mila potofu zinazochangiwa na uwepo wa
mfumo dume ambayo inaathiri ustawi wa wanawake na watoto mkoani humo.
Bi. Vicky asema kuwa Serikali ya
Mkoa wa Mara imejipanga katika kuhakikisha inatokomeza vitendo vya
kikatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo utoaji wa elimu kwa kutumia
jumbe zilizoandaliwa na mkoa kwa kutumia redio, magazeti na mikutano
ili kuipa jamii uelewa wa juu ya madhara ya vitendo vya kikatili.
Ameutaja mkakati mwingine kuwa ni
kampeni ya kila mwisho wa mwaka ambapo vitendo vya ukeketaji hufanyika
ili kuihamasisha jamii kuachana na mila porofu zinazomgandamiza mwanamke
na mtoto.
Akiwasilisha malengo ya kikao
hicho Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa
Clothilde Komba amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kujadiliana na
kupata namana bora ya kupambana na vitendo vya ukatili mkoani humo.
Akiwasilisha jumbe katika kikao
hicho Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Sebastian Kitiku amesema kuwa jumbe hizo
muhimu sana katika kuhakikisha jamii inabadilika na kuondokana na
vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
No comments :
Post a Comment